IQNA

Waislamu India

Familia katika hali ya mshtuko baada ya mwanaume Mwislamu kuuawa m Wahindu Msikitini India

20:39 - September 16, 2023
Habari ID: 3477609
NEW DELHI (IQNA) - Familia ya Nurul Hassan, mhandisi Mwislamu katika jimbo la Maharashtra nchini India, iko katika hali ya mshtuko baada ya kuuawa kwake kikatili na kundi la Wahindu kwenye msikiti.

Mke wake, Aisha ana ujauzito wa miezi saba na amekuwa hana faraja kwa siku nne sasa.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 29 amekuwa akipuuza afya yake na ameacha kula vizuri huku akiomboleza kufiwa na mumewe, Nurul Hassan, aliyeuawa baada ya kundi la Wahindu kushambulia msikiti katika kijiji cha Pusesavali wilayani Satara ya Maharashtra.

"Ulimwengu wangu wote ulivunjika nilipoona maiti ya mwanangu kitandani. Wakati huo, sikuamini kilichokuwa kikiendelea mbele ya macho yangu,” amesema Hassan Mohammad Liyaqat, baba ya mareheni katika mazungumzo na  Al Jazeera kwa njia ya simu.

Yapata saa mbili unusu usiku wa Septemba 10, Hassan, mhandisi wa ujenzi mwenye umri wa miaka 31, aliondoka nyumbani kwake kwa ajili ya Sala ya Isha kwenye msikiti wa karibu. Mjomba wake Mohammad Siraj alisema kulikuwa na waumini wapatao 15 msikitini na Sala ilikuwa ikiendelea waliposikia zogo nje.

Umati wa watu ulikuwa umeuzunguka msikiti huo, huku wakiimba kauli mbiu dhidi ya Uislamu na kutoa matamshi ya uchochezi kuhusu Uislamu. "Takriban wanaume 150-200 wa Kihindu walikusanyika nje ya msikiti na kuanza kurusha mawe, na kuharibu baadhi ya magari yaliyokuwa yameegeshwa," alisema.

Shahidi aliyetaka jina lake lisitajwe aliiambia Al Jazeera umati wa watu ulivunja mlango wa msikiti na kuingia ndani.

"Walibeba silaha zenye ncha kali, fimbo za chuma, vipande vidogo vya granite na virungu. Walipoingia tu, walianza kuwashambulia watu wote waliokuwepo. Hassan alipigwa na chuma kichwani mara kadhaa na  eneo alimoanguka lilikuwa  dimbwi la damu. Alikuwa tayari amekufa tulipomnyanyua kutoka mahali hapo,” alisema na kuongeza kuwa takriban watu wengine 14 walipata majeraha.

Shahidi huyo alieleza zaidi jinsi kundi hilo lilivyochoma moto duka la karibu na kuharibu magari na mikokoteni yenye majina ya Kiislamu. "Waliharibu taa zote msikitini, wakachoma Qur’ani Tukufu  na vitabu vingine vya kidini, na walionekana kuwa na nia ya kutuua sisi sote," aliiambia Al Jazeera.

Siraj alisema mtu mmoja kutoka kijijini hapo alitoa taarifa kwa kituo cha polisi kilichokuwa karibu na ni kutokana na kuingilia kati ndipo genge hilo la Wahindu lilipondoka eneo la tukio. Wakati wakiondoka, magaidi hao wa Kihindu walivunja vioo vya magari yaliyokuwa yameegeshwa nje ya msikiti mwingine kijijini hapo na kutoa matamshi ya dharau kuhusu wanawake wa Kiislamu, alisema.

Mohammad Aslam Gazi, rais wa Chama cha Kulinda Haki za Kiraia, alisema katika kipindi cha miezi michache iliyopita, eneo la Kolhapur huko Maharashtra lilishuhudia ongezeko la mashambulizi dhidi ya Waislamu yanayofanywa na baadhi ya makundi ya Kihindu.
"Matukio haya yanaonekana kupangwa vyema na kuratibiwa na baadhi ya waeneza chuki, pengine kutokana na uchaguzi ujao, kwani wanalenga kupata kura kwa misingi ya hitilafu za kijamii," aliiambia Al Jazeera.

3485183

Habari zinazohusiana
Kishikizo: india waislamu
captcha