IQNA

Ahadi ya Kweli

Iran yashambulia utawala wa Israel kulipiza kisasi ugaidi

11:39 - April 14, 2024
Habari ID: 3478681
IQNA- Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limefanya mashambulizi makubwa ya kulipiza kisasi kwa kutumia makombora na ndege zisizo na rubani na makombora dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel likijibu mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa utawala wa Israel ya tarehe 1 Aprili dhidi ya majengo ya kidiplomasia ya Jamhuri ya Kiislamu katika mji mkuu wa Syria, Damascus.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran limetangaza mashambulizi hayo katika taarifa yake usiku wa kuamkia leo na kuitaja operesheni hiyo kuwa ni "Operesheni Ahadi ya Kweli."

"Katika kukabiliana na jinai nyingi za utawala wa Kizayuni, ikiwa ni pamoja na shambulio la sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran huko Damascus na kuuawa shahidi baadhi ya makamanda na washauri wa kijeshi wa nchi yetu huko Syria, Idara ya Anga ya IRGC imerusha makumi ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya baadhi ya malengo ndani ya maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel,” imesema taarifa hiyo.

Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Mohammad Reza Ashtiani, ameonya kwamba "nchi yoyote ambayo intafungua ardhi au anga yake kwa Israel kwa ajili ya kuishambulia Iran, itapata majibu yetu madhubuti."

Shambulio la Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus lilisababisha kuuawa shahidi Brigedia Jenerali Mohammad Reza Zahedi, kamanda wa Kikosi cha Quds cha IRGC, naibu wake, Jenerali Mohammad Hadi Haji Rahimi, na maafisa watano walioandamana nao.

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ametangaza katika barua kwa Baraza la Usalama kwamba ikiwa utawala wa Israel utaanzisha tena mashambulizi yoyote ya kijeshi, bila shaka jibu la Iran litakuwa la nguvu na kali zaidi.

Amir Saeed Iravani, Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ametangaza katika barua rasmi kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Rais wa Baraza la Usalama kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huku ikionya dhidi ya uchokozi wowote zaidi wa kijeshi wa utawala wa Israel, iko na azma isiyoyumba ya kujilinda na kutoa jibu kali kwa mujibu wa sheria za kimataifa, dhidi ya tishio au uchokozi wowote dhidi ya wananchi, mamlaka na mipaka yake yote.

Maelezo kuhusu silaha ilizotumia Israel katika hujama dhidi ya Israel

Jumamosi mida ya saa tano usiku kwa saa za Iran au nne na nusu usiku kwa saa za Afrika Mashariki, kitengo cha anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kilianzisha rasmi operesheni ya kulipiza kisasi dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel, na kuanzisha mawimbi manne ya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani.

Wimbi la kwanza lilijumuisha makumi ya ndege zisizo na rubani aina ya Shahed-136 za kamikaze au zinazojiangamiza, zilizokadiriwa kuwa takriban 100. Wanaharakati wa mitandao ya kijamii walipiga picha ndege hizo zikiwa katika anga za Iran na Iraq.

Shahed-136 ni ndege isiyo na rubani inaoweza kuruka umbali wa kilomita 2,000 na hubeba bomu lenye uzto wa kilo 50.

Bado haijatangazwa rasmi ni aina gani za makombora ambayo Iran ilitumia a katika operesheni hiyo yenye mafanikio makubwa, ingawa angalau baadhi ya makombora hayo yaliripotiwa kuwa Kheibar Shekan.

Kheibar Shekan ni kombora la balestiki la masafa ya kati na lina uwezo wa kuruka kilomita 1,450 husheheni bomu lenye uzito wa kilo 500.

Iran haijatangaza rasmi maeneo yaliyolengwa, nao utawala wa Kizayuni wa Israel umeamuri watu  kutosambaza video za mashambulizi ya Iran.  

Kama ilivyoelezwa kwa usahihi katika uchambuzi wa tovuti ya Press TV, shabaha kuu zilikuwa vituo vya kijeshi vya utawala wa Kizayuni, kuanzia Miinuko ya Golan hadi Jangwa la Negev.

Scott Ritter, mtaalam wa kijeshi wa Marekani, alisema kwenye jukwaa la X (zamani lilijulikana kama Twitter) kwamba angalau makombora saba ya hypersonic ya Iran yalilenga kituo cha jeshi la anga la Israel la Nevatim Air Base na hakuna hata kombora moja lililotunguliwa.

Kambi hii ya jeshi la anga iko katika jangwa la Negev na inahifadhi ndege za Kimarekani za F-35 ambazo zilitumiwa na jeshi katili la Israel katika shambulio la kigaidi kwenye ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus.

3487926

 

 

Habari zinazohusiana
captcha