IQNA

Turathi za Kiislamu

Msahafu wa zama za Uthmaniyya kupigwa mnada jijini London

20:31 - April 24, 2024
Habari ID: 3478726
IQNA – Msahafu wa kipekee wa enzi za Uthmaniyya ni miongoni mwa bidhaa za sanaa za Kiislamu zitakazopigwa mnada Sotheby's London wiki hii.

Kituo cha kupiga mnada cha Sotheby's London leo kina mnada  wa athari za sanaa ya Kiislamu na Kihindi ambazo zimekusanywa kwa zaidi ya miaka 40.

Nakala hiyo ya Qur'ani ya zama za Uthmaniyya iliagizwa na Munire Sultan, binti ya Sultan Abdulmejid wa Kwanza wa Utawala Uthmaniya, na iliandikwa na mtaalamu wa kaligrafia  Ibrahim Hakki. Tarehe iliyoandikwa katika msahafi huo mo 19 Rabi' I 1277 Hijria Qamaria (Oktoba 5, 1860 MIladia) na inaonyesha tamaduni tajiri za kisanii za Ufalma wa Uthmaniyya.

Nakala hiyo ina kipimo cha sentimita 37.9 kwa 26.4 na inajumuisha kurasai 256. Kila ukurasa una mistari 15 ya hati maridadi ya naskh, iliyoainishwa vyema kwa dhahabu.

Wataalamu wa Sotheby wanakadiria bei ya mnada ya Msahafu huo wa kipekee kuwa kati ya $86,700 na $111,400.

Mnada huo unatarajiwa kuvutia wakusanyaji na wapenda shauku ya kupata kipande cha historia cha  urithi wa Kiislamu maeneo mbalimbali kutoka Afrika Kaskazini hadi Uchina

3488060.

captcha