IQNA

Waislamu India

Mahakama ya India yasitisha ubomoaji wa Mali za Waislamu huko Nuh

17:42 - August 09, 2023
Habari ID: 3477407
NUH (IQNA) - Mahakama ya India imeuliza kama ubomoaji wa nyumba na biashara za wakazi hasa Waislamu katika jimbo la kaskazini la Haryana ni "zoezi la maangamizi ya kimbari".

Wakati wa kuamuru kusitishwa kwa siku nne za bomoa bomoa katika wilaya ya Nuh, Punjab na Mahakama Kuu ya Haryana Jumatatu ilisema, "Suala pia linaibuka ikiwa majengo ya jamii fulani yanabomolewa chini ya kisingizio cha sheria na shida ya utaratibu,  zoezi la maangamizi ya kimbari linaendeshwa na serikali.”

Benchi la Jaji GS Sandhawalia na Jaji Harpreet Kaur Jeewan pia liliona kwamba mamlaka ya serikali ilikuwa imeendesha zoezi la kubomoa "bila kufuata utaratibu uliowekwa na sheria" au kutoa arifa zozote za awali kwa watu wanaomiliki mali, tovuti ya habari ya kisheria LiveLaw iliripoti.

Mamia ya nyumba na maduka yabomolewa huko Haryana ya India

Ripoti za Jumatatu zilisema kwamba serikali ya mtaa huko Haryana ilibomoa mamia ya nyumba, maduka na vibanda katika Nuh, wilaya pekee yenye Waislamu wengi katika jimbo hilo.

Katika miaka ya hivi karibuni, makundi kadhaa ya haki za binadamu yamelaani serikali huko kwa kufanya ubadhirifu wa mali zinazomilikiwa na washukiwa hasa Waislamu katika visa vya ghasia - na hata wapinzani wa kisiasa - kuwa jambo la kawaida katika majimbo yanayoongozwa na chama cha mrengo wa kulia.

3484698

Habari zinazohusiana
Kishikizo: india waislamu
captcha