IQNA

Wanamichezo Waislamu

Kocha Mfaransa asilimu Algeria akiwa amevutiwa na mapambano ya Wapalestina

10:09 - April 28, 2024
Habari ID: 3478748
IQNA – Patrice Beaumelle, kocha wa soka wa Ufaransa ambaye kwa sasa anaongoza timu ya Mouloudia d'Alger katika ligi kuu ya soka ya Algeria, amesilimu.

Tangazo hilo lilikuja baada ya Beaumelle, anayejulikana kwa muda wake kama kocha msaidizi wa Herve Renard, kushiriki katika sherehe ya kusilimu katika msikiti wa Djenane Mabrouk huko El Harrach, Algiers.

Baada ya Swala ya Ijumaa, alitamka Shahada, akibainisha imani yake mpya.

Klipu iliyosambaa mitandaoni inayomuonyesha kocha huyo akiwa msikitini alionyesha furaha yake na "fahari" kuhusu uamuzi wake wa kusilimu na hivyo kukumbatia Uislamu maishani.

Imamu wa msikiti huo pia alihutubia waumini, akibainisha kwamba Beaumelle alitiwa moyo na Muqawama (mapambano ya Kiislamu) wa watu wa Palestina.

Beaumelle alisilimu kwa sababu aliathiriwa na mapambano ya taifa la Palestina wakati wa kukabiliana na mashambulizi ya mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel.

Kocha huyo aliukubali Uislamu alipokuwa akifanya uchunguzi kuhusu siri ya mapambano ya Wapalestina dhidi ya jinai za Israel, Iamu huyo aliongeza.

Safari ya soka ya Beaumelle inajumuisha majukumu kama mlinzi katika siku zake za uchezaji na safu ya nafasi za juu za ukocha. Amefanya kazi kwa karibu na Renard katika timu kadhaa, ikiwa ni pamoja na timu za taifa za Angola, Zambia, na Ivory Coast, na ameshikilia nafasi ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ivory Coast kabla ya kuinoa Algeria.

3488111

captcha