IQNA

Turathi

Nakala Adimu ya Qur'ani ya Karne ya 15 katika Maonyesho ya Vitabu ya Abu Dhabi

17:27 - May 25, 2023
Habari ID: 3477045
TEHRAN (IQNA) – Nakala adimu ya Qur'ani Tukufu ya karne ya 15 Miladia ni miongoni mwa vitu vilivyoonyeshwa kwenye Maonyesho ya Vitabu ya Abu Dhabi 2023 katika Umoja wa Falme za Kiarabu.

Shirika la  Vitabu Adimu na Maandishi, ambalo linajishughulisha na vitabu adimu ndilo lililowasilisha  Msahafu huo nadra unaokadiriwa kuwa na thamani ya euro 85,000, sawa na dirham 336,595, kwenye banda lake.

Mohammed Asif ambaye ni mmiliki wa kampuni hiyo ameeleza kuwa kuwa kampuni hiyo inamilizi hati asili ikiwemo Misahafu zaidi ya 600 ya karne nne zilizopita.

Mwezi Agosti mwaka 2021, Sheikh Sultan Bin Mohammed Al Qasimi, Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Mtawala wa Sharjah, alikabidhi nakala nne nadra za nakala za Qur'ani Tukufu kwa Akademia ya Qur'ani Tukufu mjini Sharjah.

Misahafu hiyo nadra ni ya kutoka kipindi cha watawala wa Iran wa silsila ya Ilkhanid katika karne ya saba Hijria Qamaria. Misahafu inanasibishwa na  mwandishi hati maarufu Yaqut Al Musta'simi.

3483683

Kishikizo: msahafu qurani nadra uae
captcha