IQNA

Wachapishaji Msahafu wa Kitaifa UAE waenziwa

19:57 - August 09, 2021
Habari ID: 3474174
TEHRAN (IQNA)- Taasisi ya Tuzo ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Dubai imewaenzi wachapishaji na wasambazaji Misahafu katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Taasisi ya Kimataifa ya Tuzo ya Kurani Tukufu Dubai iliandaa sherehe ya kukamilisha uchapishaji wa toleo la kwanza la Msahafu wa Kitaifa wa UAE.

Ibrahim Mohammed Bomleha, Mshauri wa Mtawala wa Dubai na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Taasisi ya Kimataifa ya Tuzo ya Qur’ani Tukufu Dubai na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Mushaf ya Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan, alizungumza katika sherehe hiyo.

"Msahafu uliochapishwa, ambao sote tunajivunia, umefika hapa kufiatia  agizo la Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, Naibu Waziri Mkuu na Mtawala wa Dubai.”

Mshauri wa mtawala wa Dubai alisema: "Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu, tangu mwanzo ilikuwa na azma ya kuchapisha Mus'haf  wa kitaifa wa UAE, na hivyo tulichagua wajumbe wa kamati ya utawala inayosimamia kazi hii.” Amesema kazi hiyo ilisimamiwa na wasomi pamoja na wataalamu wa Qur’ani Tukufu.

3989178

Kishikizo: dubai msahafu
captcha