IQNA

Ka'aba Tukufu

Kazi ya kukarabati Ka’aba Tukufu

6:31 - December 12, 2023
Habari ID: 3478023
IQNA – Mpango wa kawaida wa matengenezo na ukarabati wa Ka’aba katika mji mtakatifu wa Makka ulianza Jumamosi.

Mpango huo unatekelezwa chini ya uratibu wa Idara ya  Usimamizi wa Miradi katika Wizara ya Fedha ya Saudia kwa ushirikiano na mashirika ya serikali yanayohusiana, tovuti ya Youm7 iliripoti.

Katika mpango huo kutakuwa na kazi ya matengenezo na kuhakikisha eneo hilo takatifu linabakia katika hali bora zaidi kwa ajili ya kuwapokea wageni wa Mwenyezi Mungu.

Teknolojia za hivi karibuni zinatumiwa kuhakikisha viwango vya juu zaidi katika utekelezaji wa kazi ya matengenezo, maafisa wanasema.

Tangu kuanzishwa kwake, Idara ya  Usimamizi wa Miradi katika Wizara ya Fedha ya Saudia imepewa jukumu la kusimamia mipango ya maendeleo katika Msikiti Mkuu wa Makka na Msikiti wa Mtume huko Madina.

Miradi ya miaka ya hivi karibuni ya kupanua zaidi  Msikiti Mkuu wa Makka (Masjid al-Haram), imekosolewa na baadhi ya wataalam wa dini na turathi ambao wanasema miradi hiyo  imebadilisha utambulisho wa kihistoria wa eneo hilo takatifu na kusababisha uharibifu wa usanifu majengo wa kihistoria msikiti huo.

Video na picha zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha kizuizi kilichowekwa karibu na Kaaba kwa ajili ya kazi ya matengenezo na wafanyakazi wanaweza kuonekana wakifanya kazi zao huku waumini wakiendelea na Ibada.

Kazi ya ukarabati inahusisha kukarabati bomba la kupitishia maji ya mvua, kufunika paa kwa marumaru, na kurekebisha milango.

Watch: Saudi Arabia begins periodic maintenance for Holy Kaaba

Kishikizo: kaaba masjid haram kiswa
captcha