Waumini wakiwa wamevalia mavazi meupe ya Ihramu, na baadhi wakiwa na mwavuli wa kujikinga na jua kali, wametukfu au kuzunguka Kaaba tukufu katika Msikiti Mkuu wa Makka.
" Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu.... haiwezekani kuelezea hisia zangu hivi sasa," Ahmed Sayed Mahmoud, amesema hujaji kutoka Misri. "Kuwa katika Msikiti Mkuu wa Makka na katika ardhi hii ya Misikiti Miwili takatifu kunanifurahisha sana."
Kuna misikiti miwili mitakatifu zaidi katika Uislamu Saudi Arabia, ambayo ni Msikiti Mkuu wa Makka, Al Masjid Al Haram mjini Makka na Al-Masjid an-Nabawi mjini Madina. Mwaka huu Saudia imeruhusu Waislamu kutoka nje ya ufalme huo kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu baada ya miaka miwili.
Ni raia elfu chache tu wa Saudia na wakaazi wa kigeni nchini humo walihudhuria Hija ya kila mwaka katika miaka miwili iliyopita wakati Covid-19 ilisababisha shida katika usafiri duniani
Mwaka huu ni Waislamu milioni moja tu watakaotekeleza ibada ya Hija, chini ya nusu ya viwango vya kabla ya Covid, na wanaoruhusiwa ni wenye umri wa miaka 18 hadi 65 ambao wamechanjwa kikamilifu na hawana magonjwa sugu. Waumini wataendelea kuingia Saudia kabla ya kuanza ramsi ibada ya Hija siku chache zijazo.
3479527