IQNA

Ta'azia

Msomaji mashuhuri wa Ibtihal nchini Misri Zia al-Nazir aaga dunia

6:06 - December 12, 2023
Habari ID: 3478022
IQNA – Sheikh Zia al-Nazir, msomaji maarufu wa Ibtihal nchini Misri, alifariki dunia Jumamosi, Desemba 9.

Alikuwa msomaji rasmi wa Ibtihal wa Redio ya Kurani ya Misri, kulingana na Al-Misri Al-Yawm kila siku.

Ibtihal ni kisomo cha dua na mashairi hasa ya  kumsifu Mtukufu Mtume (SAW). Ibthihal ni maarufu katika nchi nyingi za Kiarabu, haswa Misri, na idadi kubwa ya maqarii wa Qur'ani Tukufu ni maarufu pia kwa usomaji wao wa Ibtihal.

Mazishi ya Zia al-Nazir yamefanyika katika kijiji chake cha Tanan katika Mkoa wa Al-Qalyubia. Baadhi ya maqarii maarufu, akiwemo Sheikh Fathullah Bibris na Sheikh Ahmed al-Fashni, wametoa rambirambi kwa kifo cha msomaji huyo wa Ibtihal, wakiomba rehema za Mwenyezi Mungu kwa ajili ya roho yake.

Hapa chini ni kisomo cha Ibtihal cha al-Nazir kilichofanywa katika hafla ya Eid al-Fitr:

4186957

captcha