IQNA

Chuki dhidi ya Waislamu

Wasiwasi wa Waislamu Ujerumani kufuatia vitisho vya Wanazi mamboleo

16:21 - May 26, 2023
Habari ID: 3477047
TEHRAN (IQNA) –Waislamu katika mji wa kati wa Ujerumani wa Goettingen wameeleza "wasiwasi" baada ya msikiti wao kupokea barua ya vitisho yenye nembo ya Kinazi ya Swastika na nembo nyinginezo za Wanazi mamboleo.

Mehmet Ibrahimbas, mwenyekiti wa Jumuiya ya Misikiti ya Goettingen, alisema barua hiyo ilikuwa na lugha ya ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Uislamu, na ilikuwa na lakabu ya Wanazi-mamboleo "NSU 2.0."

"Kuna wasiwasi katika jumuiya yetu ya misikiti na Waislamu  Goettingen kutokana na vitisho vinavyoendelea vya vurugu," alisema siku ya Alhamisi, na kuongeza kuwa hiyo ni barua ya pili ya vitisho waliyopokea katika miezi kadhaa.

Mnamo Septemba mwaka jana, washukiwa wasiojulikana pia walipaka rangi ya swastika kwenye ukuta wa msikiti huo, unaoendeshwa na taasisi ya  Kituruki-Kiislamu  yaDITIB.

"NSU 2.0" inamaanisha  National Socialist Underground, kundi la kigaidi la Wanazi mamboleo lililofichuliwa mwaka 2011 ambalo liliua watu 10 na kufanya mashambulizi ya mabomu yaliyolenga wahamiaji.

Ujerumani imeshuhudia kuongezeka kwa ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Uislamu katika miaka ya hivi karibuni, ikichochewa na propaganda za makundi ya mrengo wa kulia, ambayo yametumia vibaya mzozo wa wakimbizi na kujaribu kuzua hofu kwa wahamiaji.

Kulingana na data ya hivi punde, polisi walisajili angalau vitendo vya uhalifu 610 vya chuki dhidi ya Uislamu mnamo 2022 kote nchini.

Takriban misikiti 62 ilishambuliwa kati ya Januari na Disemba mwaka jana, na takriban watu 39 walijeruhiwa kwa sababu ya ghasia dhidi ya Waislamu.

Takwimu hizo pia zilijumuisha makumi ya uhalifu wa chuki dhidi ya Waislamu, visa vya vitisho, na uharibifu wa mali.

Nchi ya watu zaidi ya milioni 84, Ujerumani ina idadi ya pili ya Waislamu katika Ulaya Magharibi baada ya Ufaransa. Ni nyumbani kwa Waislamu karibu milioni 5, kulingana na takwimu rasmi.

3483704

captcha