IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu Ujerumani

Wito wa kuidhinishwa sheria za kukabiliana na chuki dhidi Uislamu Ujerumani

6:42 - February 26, 2024
Habari ID: 3478416
IQNA - Mbunge mmoja nchini Ujerumani ametoa wito wa kujumuishwa kwa sheria za kupinga Uislamu katika katiba ya nchi

Kulingana na tovuti ya habari ya Exberliner, mbunge mwandamizi Raed Saleh Saleh anataka sheria za kupinga chuki dhidi ya Uislamu zijumuishwe pamoja na vipengee vya kikatiba vinavyokabiliana na chuki dhidi ya Wayahudi.

Saleh, ambaye ni kiongozi wa chama cha Social Democratic Party, alisisitiza haja ya Ujerumani kuwa na katiba inayoonyesha kwa nguvu nia na dhamira ya nchi hiyo kukabiliana na dhidi ya chuki dhidi ya Wayahudi, chuki dhidi ya Uislamu na ubaguzi wa rangi.

"Ninaweza kuoana hapa Berlin tukisema kwamba katika jiji letu lenye watu wa jamii mbali mbali tutakabiliana na  chuki dhidi ya Wayahudi, tutakabiliana na chuki dhidi ya Uislamu na pia tutakabiliana na ubaguzi wa rangi katika katiba,” alisema.

Matamshi hayo yanakuja huku kukiwa na ongezeko la kasi na la kutisha la mashambulizi ya chuki dhidi ya Uislamu nchini Ujerumani na sehemu kubwa ya Ulaya, huku ripoti zikionyesha kuongezeka kwa vitendo vinavyowalenga Waislamu na taasisi za Kiislamu kama vile misikiti.

Jumuiya za Waislamu nchini Ujerumani na Ulaya kwa ujumla katika miaka ya hivi karibuni zimekuwa zikikabiliana na chuki dhidi ya Uislamu inayotoka sio tu kutoka kwa raia wa kawaida bali pia kutoka kwa wanasiasa waliochaguliwa na watu wengine wenye mamlaka.

Kulingana na ripoti za hivi majuzi, polisi Ujerumani walirekodi uhalifu 258 wa chuki dhidi ya Uislamu katika nusu ya kwanza ya 2023.

Kati ya Januari na Juni mwaka jana, zaidi ya misikiti kumi ilishuhudia vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu.

Waislamu pia wamekumbana na mashambulizi ya kimwili au unyanyasaji wa maneno mitaani au katika maeneo mengine ya umma kote Ujerumani, na watu 17 wanasemekana kupata majeraha katika hujuma hizo za chuki dhidi ya Uislamu.

/3487327

Kishikizo: ujerumani waislamu
captcha