IQNA

Waislamu Ujerumani

Kiongozi wa Waislamu Ujerumani aonya kuhusu 'hali ya wasiwasi' baada ya vita vya Gaza

16:57 - November 28, 2023
Habari ID: 3477958
BERLIN (IQNA) – Kiongozi mmoja wa jamii ya Waislamu nchini Ujerumani ameelezea wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa chuki dhidi ya Waislamu nchini humo kufuatia vita vya utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina huko Gaza.

Aiman Mazyek, Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu nchini Ujerumani amesema kuwa jamii ya Waislamu katika nchi hiyo ya Ulaya inakabiliwa na mashambulizi zaidi dhidi ya misikiti na watu binafsi katika wiki zilizopita kuliko hapo awali. Aliongeza kuwa:  "Tunashuhudia mashambulizi mendi dhidi ya Waislamu na pia wale wanaochukuliwa kuwa Waislamu kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea hapo awali."

Alisema alikuwa "na wasiwasi sana" kuhusu usalama wa Waislamu nchini Ujerumani, ambao wanaweza kulengwa kwa ajili ya dini yao au sura zao.

Alitoa mfano wa shambulio la risasi huko Vermont, Marekani, ambapo Wapalestina watatu walijeruhiwa kwa kuvaa skafu ya Wapalestina na kuzungumza Kiarabu.

Serikali ya Ujerumani pia ililaani mashambulizi hayo dhidi ya Waislamu na kusema "hayakubaliki kabisa".

Msemaji wa serikali Steffen Hebestreit alisema mnamo Novemba 6 kwamba Waislamu karibu milioni 5 nchini Ujerumani walikuwa na haki ya kulindwa.

Vita vya maangamizai ya umati vya Israel dhidi ya Wapalestin huko Gaza vilianza tarehe 7 Oktoba na vimezusha maandamano na mivutano katika nchi nyingi ikiwemo Ujerumani.

Mzozo huo pia umesababisha ongezeko kubwa la hisia dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi huku wataalam wakilaumu vyombo vya habari kwa kuupendelea utawala haramu wa Israel na kueneza propaganda chafu dhidi ya Wapalestina.

3486205

Kishikizo: waislamu ujerumani gaza
captcha