IQNA

Jinai za Israel

Israel inapanga kupora maeneo ya akiolojia ya Wapalestina

19:19 - July 16, 2023
Habari ID: 3477292
AL-QUDS (IQNA) – Utawala haramu wa Israel unapanga kuteka maeneo ya kiakiolojia ya Wapalestina kote Ukingo wa Magharibi, Mamlaka ya Ndani ya Palestina (PA) ilionya.

PA imetoa wito kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kutekeleza majukumu yake katika suala hili.

Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina, kwa maneno makali, imelaani uvamizi wa Israel usiku wa Alhamisi kwenye kijiji cha akiolojia cha Sebastia.

Imelaani vikali Israel na wanamgambo wa walowezi wa Kizayuni kwa kuchukua mamlaka ya eneo hilo la akiolojia la zama za Warumi.

"Hili ni shambulio ambalo liko ndani ya mpango wa kuteka maeneo ya kiakiolojia ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kulazimisha mamlaka ya Israel katika maeneo yaliyonyakuliwa," Wizara ya Mambo ya Nje ilisema.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina ilisema: "Taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya Kiebrania zimethibitisha kwamba utawala wa Israel uko karibu kutenga mamilioni ya shekeli kwa madhumuni ya kuteka maeneo ya kiakiolojia ya Palestina."

Wizara ya mambo nje ilidokeza kuwa utekelezaji wa mpango huu ni sehemu ya hatua kwa hatua ya Israel kutwaa Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa, hususan UNESCO, kuchukua jukumu la kulinda maeneo ya kiakiolojia na urithi wa Palestina.

3484350

Kishikizo: unesco israel palestina
captcha