IQNA

Diplomasia

Rais wa Iran atembelea Haram Takatifu ya Bibi Zeynab katika safari nchini Syria

16:12 - May 04, 2023
Habari ID: 3476956
TEHRAN (IQNA) – Rais wa Iran Ebrahim Raisi, ambaye yuko katika safari rasmi nchini Syria, ametembelea kaburi takatifu la Bibi Zainab (SA) huko Damascus.

Katika ziara hiyo, Muhammed Abdul Sattar Waziri wa Wakfu wa Syria na rais wa Jumuiya ya Ahl-ul-Bayt (AS) ya nchi hiyo ya Kiarabu Abdullah Nizam katika hotuba zao waliashiria nafasi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kupambana na ugaidi na katika kuhakikisha usalama na uthabiti wa eneo hilo.

Rais pia alitoa hotuba katika mkusanyiko wa makundi tofauti ya watu, wanazuoni wa Syria kutoka madhehebu mbalimbali za fikra za Kiislamu, na familia za mashahidi, makamanda na wapiganaji wa mhimili wa upinzani.

Kabla ya kuzuru kaburi hilo takatifu, pia alifanya mazungumzo na familia za mashahidi wa Harakati  Muqawama kutoka Syria, Lebanon, Afghanistan, Iran na nchi zingine.

Raisi aliwasili Syria mapema Jumatano kwa ziara ya siku mbili yenye lengo la kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili marafiki.

Yeye na mwenzake wa Syria Bashar al-Assad walifanya mazungumzo mjini Damascus na kisha kutia saini makubaliano ya kina kuhusu ushirikiano wa muda mrefu na wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili.

Hii ni mara ya kwanza kwa rais wa Iran kutembelea nchini Syria katika kipindi cha zaidi ya miaka 13.

Haram takatifu ya Hazrat Zainab (SA) katika Kitongoji cha Zainabiya cha Damascus ni eneo la Ziyara ina hutembelewa na mamilioni ya Waislamu kutoka kote ulimwenguni kila mwaka.

Hotuba Zeinabiya

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kusimama imara mataifa ya Palestina na Syria kumebadilisha hali ya mambo kwa manufaa ya kambi ya muqawama na leo hii utawala wa Kizayuni wa Israel ni dhaifu zaidi kuliko wakati mwingine wowote.

Sayyid Ebrahim Raisi  amesema hayo wakati alipohutubia Waislamu ndani ya Haram ya Bibi Zainab SA mjini Damascus. 

Amesema, maadui wa Uislamu wamefanya njama na fitna kwa muda wa miaka 12 na wamemimina fedha nyingi haramu kuyasaidia magenge ya kikatili na kigaidi kama Daesh (ISIS) kama ambayo wametumia pia mabanda makubwa ya propaganda ya kibeberu dhidi ya taifa linalodhulumiwa la Syria, kuua watoto na wanawake wa taifa hilo na kuharibu miji na nyumba zao, lakini hivi sasa Syria imeibuka mshindi na imezidi kuwa imara. 

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, leo hii Syria inatembea kifua mbele huku maadui wa Uislamu wakiwa na kovu la milele la aibu na fedheha.

Amesema, pembeni mwa jinai za miaka 12 za Marekani na Wazayuni huko Syria na Iraq, kuna ukurasa mwingine uliojaa nuru, nao ni ukurasa wa muqawama, kusimama kidete, kujihami vilivyo mataifa hayo na kukata mikono michafu ya mabeberu ambako kumeifanya kambi ya muqawama kuwa imara zaidi.

Rais Raisi aidha amesema, wakati nchi mbili za Kiarabu na Kiislamu za Syria na Iraq zilipovamiwa na kuhujumiwa na magenge ya ukufurishaji, baadhi ya watu walishindwa kutoa tathmini sahihi, lakini Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alitoa tathmini sahihi kabisa ya njama hizo na kusema kuwa jinai hizo za Wazayuni zitashindwa, na kambi ya muqawama itazidi kuwa imara.

Iran’s President Visits Hazrat Zeynab Holy Shrine during Syria Trip

Iran’s President Visits Hazrat Zeynab Holy Shrine during Syria Trip

4138435

Kishikizo: zeynab Rais Raisi iran
captcha