IQNA

Jinai za Israel

Hamas yakosoa UNSC kwa kushindwa kulaani hujuma ya Israel huko Huwara

21:11 - March 03, 2023
Habari ID: 3476650
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa idara ya uhusiano wa kimataifa katika Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) anasema kushindwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika kushughulikia jinai iliyotendwa hivi karibuni na utawala haramu wa Israel katika eneo la Huwara ni jambo ambalo litaupa kiburi utawala huo kuendeleza jinai zake.

Basim Naim alisema kushindwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoa tamko la kulaani shambulio la kigaidi la walowezi wa Israel dhidi ya Wapalestina huko Huwara, kusini mwa Nablus, kaskazini mwa eneo la Ukingo wa Magharibi linalokaliwa kwa mabavu, "kunaimarisha sheria ya msitu na machafuko."

"Jeshi la Israel lenyewe linaelezea mashambulizi ya walowezi kuwa ni ugaidi," Naim alisema, na kuongeza kuwa   Marekani inabebe dhima ya "kimaadili na kisiasa kwa maisha ambayo yatapotezwa mikononi mwa mafashisti hawa."

Amesisitiza kuwa sera zinazofuatwa na Marekani katika miongo kadhaa iliyopita zimelinyima eneo hilo fursa yoyote ya usalama na uthabiti.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilishindwa, katika kikao chake kilichofanyika Jumanne jioni, kufikia taarifa ya kulaani mashambulizi ya walowezi wa Israel dhidi ya Wapalestina na mali zao katika mji wa Huwara.

Vyanzo vya Umoja wa Mataifa vilihusisha kutochukuliwa hatua na shinikizo kutoka kwa Marekani  ambayo ilipinga asimu ya azimio la kulaani jinai hiyo dhidi ya Wapalestina.

Siku ya Jumapili usiku, Mpalestina mmoja aliuawa, mamia walijeruhiwa na makumi ya nyumba na magari kuharibiwa katika mashambulizi ya walowezi katika mji wa Huwara na vijiji vya jirani karibu na Nablus.

3482682

captcha