IQNA

Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajioun

Kiongozi Muadhamu atoa rambirambi kufuatia kuaga dunia Ayatullah Naseri

21:05 - August 27, 2022
Habari ID: 3475686
TEHRAN (IQNA) – Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametoa salamu za rambirambi kufuatia kuaga dunia Ayatullah Mohammad Ali Naseri, mwanazuoni mashuhuri wa maadili wa Iran aliyefariki dunia Ijumaa akiwa na umri wa miaka 92.

Katika ujumbe wake siku ya Jumamosi, Kiongozi Muadhamu amemtaja Marhum Ayatullah Naseri kuwa ni mwanazuoni mwaminifu na msafiri katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Ufuatao ni ujumbe wa Kiongozi Muadhamu, kwa mujibu wa tovuti ya Khamenei.ir:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Kufuatia kuaga dunia mwanachuoni mcha Mungu na msafiri katika njia ya Mwenyezi Mungu, Ayatullah Haj Sheikh Muhammad Ali Naseri, ninawapa pole watu wote wa Isfahan, wapenzi wake wote, wale wote walionufaika na mafundisho ya marehemu, na hasa  kwa watoto waheshimiwa.

Mwanachuoni huyu mtukufu na mwalimu wa maadili aliiona kazi hii kubwa ya utakaso na kueneza mafundisho ya maadili ya Kiislamu kuwa ni wajibu wake. Kwa kunufaika na moyo wake mnyenyekevu, na wenye nuru, alitumia maneno yenye matokeo na yenye kupenya ili kutimiza kazi hiyo. Rehema na ridhaa ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake. Ninamwomba Mwenyezi Mungu, akubali huduma zake na ampe msamaha wake.

Sayyid Ali Khamenei

Agosti 27, 2022

Ayatollah Naseri alizaliwa mwaka wa 1930 huko Esfahan. Baada ya kumaliza shule ya msingi huko Dolat Abad, alihudhuria Shule ya Seminari ya Isfahan. Akiwa na umri wa miaka 14, alihamia Najaf ya Iraq pamoja na baba yake na kuendelea na masomo yake ya Kiislamu katika mji huo mtakatifu.

Alihudhuria madarasa ya wanazuoni wakuu kama vile Mohammad Kufi, Seyed Mohammad Kashmiri, Sheikh Abbas Ghouchani, Seyed Hashem Haddad, Seyed Jamaleddin Golpayegani, na Allameh Tabatabai.

Ayatullah Nasseri alikuwa akitoa mihadhara, hasa kuhusu maadili ya Kiislamu, katika Msikiti wa Kamar Zarrin huko Esfahan.

4080965

captcha