IQNA

Wamisri washinda mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Port Said

15:12 - February 24, 2022
Habari ID: 3474969
TEHRAN (IQNA)- Wawakilishi wa Misri wameshinda kategoria zote za Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Port Said.

Mashindano hayo yalianza Ijumaa wiki iliyopita na kuleta pamoja washiriki kutoka nchi 66 ambapo washinid walitangazwa Jumanne katika sherehe ya kufunga mashindano hayo.

Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouli alikuwa miongoni mwa waliohudhuria sherehe za kufunga mashidano hayo.

Kwa mujibu wa maamuzi ya jopo la majaji Islam Muhammad Ahmed Rajab kutoka Misri alishika nafasi ya kwanza katika kuhifadhi Qur'ani. Katika kitengo cha wanawake, Nura Ahmed Ahemd Basyuni na Asma Adil kwa pamoja wameshika nafasi ya kwanza. Aidha katika kitengo cha Ibtihal, nafasi ya kwanza imechukuliwa na Omar Ahmed wa Misri.

 
 

 4038318

captcha