IQNA

Kituo cha Utamaduni cha Iran, TV ya Nigeria kuandaa mashindano ya Qur’ani

23:52 - August 29, 2016
Habari ID: 3470540
Kituo cha Utamduni cha Iran nchini Nigeria kinashirikiana na al-Afrikiy Islamic TV kuandaa mashindano ya Qur’ani katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, uamuzi wa kuandaa mashindano hayo ulifikiwa siku chache zilizopita katika mkutano baina ya Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Iran mjini Abuja Bw. Saeed Omidi na Mkurugenzi wa al-Afrikiy TV , Ishaq Bayu Aduale.

Katika kikao hicho, Aduale alisema al-Afrikiy TV ilianziswha mwaka 2013 kwa lengo la kustawisha mafundisho ya Kiislamu na kuimarisha umoja miongoni mwa Waislamu. Amesema vipindi vya televisheni hiyo hurushwa nchini Nigeria na nchi zingine 19 za Afrika.

Kwa upande wake, Bw. Omidi ameipongeza televisheni hiyo kwa jitihada zake za kueneza Uislamu na akabaini kuwa Kituo cha Utamaduni cha Iran kiko tayari kushirikiana na al-Afrikiy TV kuandaa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Qur’ani nchini Nigeria.

3460860

captcha