Hafla hiyo ya kimataifa, inayojulikana kama Tuzo ya Kimataifa ya Mohammad VI, itaanza Septemba 12, wizara hiyo ilisema, kulingana na tovuti ya Ahdath Info.
Sherehe ya uzinduzi itafanyika katika Msikiti wa Hassan II huko Casablanca, ilibainisha.
Washindani watashindana katika kategoria za kuhifadhi Qur'anI, kisomo, Tarteel na Tafsir. Wahifadhi na wasomaji wa Qur'ani kutoka Morocco pamoja na nchi nyingine za Afrika, ulimwengu wa Kiarabu, Asia na Ulaya watashiriki katika mashindano hayo, wizara hiyo iliendelea kusema.
Itakuwa ni toleo la 17 la tukio la kimataifa la Qur'ani, ambalo hufanyika kila mwaka kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) kama sehemu ya juhudi za wizara hiyo kuendeleza kuhifadhi Qur'ani, Tajweed na Tafsir.
Morocco ni nchi ya Kiarabu ya Kaskazini mwa Afrika inayopakana na Bahari ya Atlantiki na Bahari ya Mediterania. Uislamu ndiyo dini kuu nchini Morocco, huku asilimia 99 hivi ya watu wakiufuata.
4162872