Mshauri ya kamati ya sera za kigeni katika Bunge la Iraq amesema wataishtaki pia Marekani kwa hatua yake ya kutumua silaha zilizopigwa marufuku katika maeneo ya raia nchini humo.
Hatif al-Rikabi amesema Iraq itawasilisha kesi hizo katika mahakama za Sweden na Ujerumani kuhusu jinai ambazo Marekani imetanda katika nchi hiyo ya Kiarabu.
Amesema kila mwezi kesi mpya za saratani hurekodiwa Iraq na ushahidi unaonyesha kuwa ugonjwa huo nchini humo unasababishwa na silaha ambazo Marekani inatumia.
Vita vya Marekani Iraq vimepelekea kuachwa mabaki ya silaha zenye madini ya urani na kemikali zigine za sumu.