IQNA

Tahadhari kuhusu mashambulizi dhidi ya vituo vya Hizbullah ya Iraq

21:50 - June 26, 2020
Habari ID: 3472900
TEHRAN (IQNA) - Hujuma ya majeshi ya kigaidi ya Marekani kwa ushirikiano na waitifaki wao Iraq dhidi ya vituo vya Brigedi za Kata'ib Hizbullah imelaaniwa vikali kote katika nchi hiyo.

Brigedi za Kata'ib Hizbullah ni sehemu ya Vikosi vya Kujitolea vya Wananchi wa Iraq yaani Al-Hashd al Shaabi.

Kwa mujibu wa taarifa, Javad al Tilbawi mmoja kati ya viongozi wa Harakati ya Asa'ib Ahl al-Haq ya Iraq amesema hujuma dhidi ya vituo vya Brigedi za Kata'ib Hizbullah ni sawa na kucheza na moto na ametahadharisha kuhusu matokeo mabaya ya kitendo hicho.

Naye Hassan Fadoun mwakilishi wa Mrengo wa Hikma katika Bunge la Iraq amesema hujuma hiyo dhidi vikosi vya Hashd al Shaabi na kukamatwa makamanda kadhaa wa vikosi hivyo ni kitendo cha kichochezi ambacho kitakuwa na matokeo mabaya.

Watumizi wa mitandao ya kijamii hasa Twitter kwa lugha ya Kiarabu wamekasirishwa na kitendo hicho cha Wamarekani na kuanzisha hashtegi kama vile "Mujahidina wetu ni mstari wetu mwekundu; huku wakitangaza kuunga mkono vikosi vya Hashd al Shaabi.

Vikosi vya kigaidi vya Markeani mapema leo Ijumaa asubuhi vikiwa na magari 40 ya deraya, na kwa himaya ya waitifaaki wao katika kikosi maalumu cha Iraq, vilishambulia kituo cha Brigedi za Hizbullah ya Iraq katika eneo la Ad Dourah mjini Baghdad na kuwakamata wanachama wasiopungua 13 wa Kataib Hizbullah.

Kitendo hicho cha kichokozi kimekabiliwa na radiamali kali ya vikosi vya Al Hashd al Shaabi ambavyo vimeingiza wapiganaji wake katika Eneo la Kijani mjini Baghdad.

Taarifa zinasema kufuatia radiamalia ya haraka ya Al Hashd al Shaabi, wanachama wa Kataib Hizbullah waliokamatwa wameachiliwa huru.

3906996

captcha