IQNA

Kadhia ya Palestina

Nchi za Amerika ya Latini zavunja uhusiano na Israel kutokana na jinai Gaza

18:40 - November 01, 2023
Habari ID: 3477826
SANTIAGO (IQNA) - Baada ya Bolivia kukata uhusiano wa kidiplomasia na utawala haramu wa Israel, nchi nyingine mbili za Amerika ya Latini zimewataka mabalizo wao walioko Israel kurejea nyumbani.

Chile na Colombia zimetaja vita vya kikatili vinavyoendelea vya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya eneo la Wapalestina la Ukanda wa Gaza kuwa sababu ya hatua hiyo. 

Mataifa ya Amerika Latini yaliwaita tena wajumbe wao siku ya Jumanne, siku ya 24 ya vita hivyo ambavyo hadi sasa vimedai zaidi ya Wapalestina 8,600.

Mashambulizi ya hivi punde zaidi ya Israel yalilenga kambi ya wakimbizi ya Jabaliya huko Gaza, na kuua na kuwajeruhi takriban Wapalestina 400, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Chile ilitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano na kupitishwa kwa misaada ya kibinadamu katika eneo la pwani, na kusema Israel inakiuka sheria za kimataifa.

Kando na mashambulizi ya mara kwa mara ya mabomu, Israel pia imezuia maji, chakula, na umeme hadi Gaza, na kulitumbukiza eneo hilo lililozingirwa katika mgogoro wa kibinadamu.

Rais wa Colombia Gustavo Petro aliyataja mashambulizi ya Israel kuwa "mauaji makubwa ya watu wa Palestina" katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Mapema siku hiyo, Bolivia ilikata uhusiano wake wa kidiplomasia na Israel kutokana na jinai za utawala wa Tel Aviv dhidi ya binadamu.

Aidha  Mexico na Brazil, pia zimetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano.

Akizungumza siku ya Jumatano, Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva alisema kinachoendelea Gaza mikononi mwa utawala wa Israel "sio vita. Ni mauaji ya kimbari..."

"Kusema ukweli, sijui jinsi mtu anaweza kuingia vitani akijua kwamba matokeo ya vita hivyo ni kifo cha watoto wasio na hatia," aliongeza.

"Kusema ukweli, sijui jinsi mtu anaweza kuingia vitani akijua kwamba matokeo ya vita hivyo ni vifo vya watoto wasio na hatia," aliongeza.

Rais wa Brazil alionya kwamba matukio ya sasa katika Mashariki ya Kati (Asia Magharibi) ni "hatari", akiongeza kuwa suala hilo si suala la kujadili "nani sahihi na nani asiyefaa, nani alipiga risasi ya kwanza na nani aliyefyatua ya pili."

3485828

Habari zinazohusiana
Kishikizo: gaza palestina
captcha