IQNA

Kadhia ya Gaza

Wanaharakati 1,000 kufikisha misaada ya kibinadamu Gaza kwa meli

17:59 - April 20, 2024
Habari ID: 3478704
IQNA-Maandalizi yanaendelea na Muungano wa Kimataifa wa Msafara wa Meli wa Uhuru, unaoundwa na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka nchi kadhaa, ili kupeleka misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza unaokabiliwa na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala haramu wa Israel.

Maandalizi hayo yanaendelea kwenye meli iitwayo Mediterranean, meli ya kubeba misaada ya kibinadamu inayohitajika sana Gaza.

Wahusika wa msfara huo wamehutubia  waandishi wa habari Istanbul, Uturuki  na kusema takriban watu 1,000 wanatarajiwa kushiriki katika juhudi hiyo kubwa ya kutuma misaada

Akizungumza katika mkutano uliohudhuriwa na wanaharakati kutoka nchi kadhaa zikiwemo Ujerumani, Malaysia, Palestina, Norway, Argentina, Hispania, Canada, na Afrika Kusini, mwanajeshi mstaafu wa Marekani na mwanadiplomasia wa zamani Ann Wright alisema kuwa walianza juhudi za Gaza mwaka 2010 katika msafara uliojumuisha Meli ya Marmara na meli nyingine saba, pamoja na washiriki kutoka mataifa kadhaa. Amesema wameanza tena mkakati wa kutuma misaada ya kibinadamu Gaza.

Ikumbukwe kuwa Mwezi Mei mwaka 2010 makamondoo wa Jeshi la Majini la Israel walishambulia meli ya Marmara ya Uturuki iliyokuwa ikikaribia pwani ya Gaza ikiwa na misaada ya kimataifa ya kibinadamu na kuwaua au kuwajeruhi makumi ya wanaharakati wa haki za binadamu waliokuwemo. Aidha mwaka 2015 askari katili wa Israel walishambulia meli ya Marianne kutoka Sweden iliyokuwa na misaada ya kibinadamu kwa ajili ya watu wa Gaza na kuitwaa. Meli hiyo ilikuwa sehemu ya msafara wa meli kadhaa za kuvunja mzingiro wa Gaza uliopewa jila la Freedom Flotilla III.

Utawala wa Israel ulianzisha mashambulizi ya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 7, 2023.

Zaidi ya Wapalestina 34,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, wameuawa huko Gaza, na wengine zaidi ya 76,800 wamejeruhiwa katika kampeni hiyo ya ukatili wa utawala dhalimu wa Israel.

3488002

Kishikizo: meli gaza misaada israel
captcha