IQNA

Al-Masjid an-Nabawi

Huduma maalum kwa Waislamu Milioni 5.2 wanaotembelea Msikiti wa Mtume (SAW)

20:54 - March 17, 2024
Habari ID: 3478532
IQNA – Msikiti wa Mtume (SAW) Al-Masjid an-Nabawi katika mji wa Madina nchini Saudia ulishuhudia Waislamu wengi wakitiririka katika siku za kwanza za mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu, huku zaidi ya waumini milioni 5.2, wakiwemo wanaoshiriki Hija ndogo ya Umrah wakiingia katika msikiti huo kwa ajili ya Sala za kila siku.

Mamlaka ya Kuu ya Masuala ya Al-Masjid an-Nabawi ilitoa huduma za kina za kuwahudumia Waislamu waliofika katika eneo hilo la pili kwa utakatifu katika Uislamu.

Ripoti iliyotolewa na Uongozi Mkuu wa Masuala ya Msikiti wa Mtume imebaini huduma nyingi zinatolewa kwa waumini wakiwemo raia wa kigeni katika wiki ya kwanza ya Ramadhani kwa mwaka wa 1445 Hijria.

Mamlaka hiyo ilibainisha kuwa zaidi ya wageni 414,878 walipata heshima ya kumzuru Mtume Muhammad (SAW) katika kipindi hicho.

Zaidi ya hayo, wageni 134,447 wanaume na 107,697 wageni wa kike walifanya walisali katika Al Rawdah Al Sharifah.

Huduma maalum zilisaidia wazee na walemavu 10,482 katika wiki iliyopita. Zaidi ya hayo, huduma za mawasiliano katika lugha nyingi zilitolewa kwa wageni 110,412 kutoka mataifa mbalimbali.

Huduma za elimu za maktaba ya Msikiti zilitumiwa na wageni 12,279, wakati maeneo ya maonyesho na jumba la makumbusho yalivutia wageni 4,567.

Zaidi ya hayo, zawadi mbalimbali 149,149 zilitolewa kwa wageni, pamoja na huduma za mwongozo na nasaha 648,411 zilitolewa kupitia nambari zilizounganishwa na njia za mawasiliano, kama sehemu ya huduma zinazopatikana kwa waumini wanaofika katika Al-Masjid an-Nabawi.

Huduma eneo la nje zilijumuisha kutoa mwongozo kwa wageni 94,814 na kuwezesha harakati kati ya ua na lango la Al-Masjid an-Nabawi kwa wageni 36,172 zaidi.

Aidha  chupa 144,000 za maji ya Zamzam zilisambazwa miongoni mwa waumini sambamba na milo ya futari15,243 kwa watu waliofunga katika maeneo yaliyotengwa ndani ya msikiti.

3487595

Habari zinazohusiana
captcha