IQNA

Waislamu Marekani

Historia baada ya Adhana kwa vipaza sauti katika Misikiti ya New York

21:20 - September 02, 2023
Habari ID: 3477539
NEW YORK (IQNA) – Kwa mara ya kwanza katika historia, mwito wa Kiislamu kwa sala, unaojulikana kama Adhana, ulisikika katika mitaa ya Jiji la New York siku ya Ijumaa.

Waislamu wengi waliohudhuria sala ya Ijumaa katika katika Kituo cha Utamaduni cha Kiislamu cha New York (ICCNY) huko Manhattan, moja ya misikiti mikubwa zaidi ya jiji hilo walikuwa miongoni mwa walioshuhudia historia hiyo. Walirekodi adhana kwa simu zao za rununu na kusambaza furaha na shukrani zao kwenye mitandao ya kijamii.

Adhana hiyo ilitangazwa kupitia kipaza sauti cha misikiti, kufuatia mwongozo mpya uliotolewa na Meya Eric Adams siku ya Jumanne. Mwongozo huo unairuhusu misikiti na nyumba zingine za ibada kuadhini siku ya Ijumaa na wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, mradi tu zisizidi desibel 54.

"Kwa muda mrefu sana, kumekuwa na mkanganyiko kuhusu ni jamii zipi haziruhusiwi kutangaza wito wao wa maombi," Adams alisema katika mkutano wa wanahabari uliohudhuriwa na wawakilishi kutoka vyama mbalimbali vya misikiti na taasisi za Kiislamu. "Leo tunasema wazi kwamba misikiti na nyumba za ibada ziko huru kutangaza mwito wao wa kusali Ijumaa na wakati wa Ramadhani bila kibali muhimu," aliongeza.

Chini ya mwongozo mpya, msikiti unaweza kutangaza adhana kila Ijumaa kati ya saa sita na nusu hadi saa saba na nusu mchana na vile vile kabla wa futari kila jioni wakati wa mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Viongozi kutoka jamii ya Kiislamu walitoa shukrani kwa meya na maafisa wengine. Mkutano ulipomalizika, kuliadhiniwa kwenye jukwaa sambamba na maelezo ya Kiingereza ya maana ya maneno ya Adhana.

Viongozi kutoka jumuiya ya Kiislamu walitoa shukrani kwa Meya na maafisa wengine kwa msaada wao na utambuzi wa haki zao za kidini na mila. Pia waliwashukuru majirani na vikundi vingine vya kidini kwa uvumilivu na mshikamano wao.

Adhana ni ibada inayowaalika Waislamu kutekeleza sala zao tano za kila siku. Inajumuisha misemo inayotangaza upweke wa Mwenyezi Mungu, utume wa Muhammad (SAW), na wakati wa sala. Adhana kwa kawaida husomwa na muadhini, au mtu anayeita kwenye swala, kutoka kwenye mnara au mnara uliounganishwa na msikiti.

Kishikizo: adhana marekani
captcha