IQNA

Waislamu Uingereza

Waislamu wa Lancaster waleta pamoja jamii kupitia michezo

14:43 - August 11, 2023
Habari ID: 3477415
LONDON (IQNA) – Jamii ya Kiislamu ya Lancaster (LICH) nchini Uingereza inaandaa mashindano ya kandanda mwezi Septemba ili kuunganisha watu kutoka asili na tamaduni tofauti.

Michuano hiyo itashirikisha timu sita za wachezaji wa rika mbalimbali, wakiwemo wakongwe na wakimbizi. Mashindano hayo yanalenga kukuza afya, kazi ya pamoja na moyo wa ushirikiano wa kjamii.

Mratibu wa mashindano hayo, Imtiaz Khoda, alisema: "Kwa kuleta wachezaji kutoka asili tofauti kwenye uwanja mmoja, mashindano yatahimiza mwingiliano wa jamii kati ya idadi ya Waislamu inayoongezeka ya jiji."

 Aliongeza kuwa mashindano hayo yanaungwa mkono na wafanyabiashara wa ndani na yanalenga kukuza uchumi na kuimarisha uhusiano kati ya jamii ya Kiislamu na jamii pana ya Lancaster.

"Pamoja, tunaweza kuangazia matokeo chanya ambayo michezo inaweza kuwa nayo katika ujenzi wa jamii na kukuza jamii inayowaleta watu pamoja zaidi. Tunaamini kwamba kuonyesha umoja na ukuaji wa jumuiya ya Waislamu huko Lancaster kupitia mashindano haya kutatumika kama ishara yenye nguvu ya ushirikishwaji na umoja, na hivyo kukuza hali ya kuwa washiriki kwa washiriki wote," amenukuliwa akisema na gazeti Lancaster Guardian.

Lancaster ni jiji lenye mandhari mbalimbali ya kidini. Kulingana na sensa ya 2021, Wakristo ni 51.8% ya idadi ya watu, wakati Waislamu wanaunda 1.9%, au watu 2,663.

captcha