IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Siku ya Kimataifa ya Quds ni kumbukumbu ya Imam Khomeini na nembo ya uhai wa Iran

18:25 - April 07, 2023
Habari ID: 3476829
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds ni kumbukumbu ya Imam Khomeini (MA) na nembo ya kuwa hai tafa la Kiislamu la Iran.

Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema hayo leo mbele ya hadhara kubwa ya waumini waliohudhuria ibada ya kisiasa na kimaanawi ya Swala ya Ijumaa mjini Tehran na kueleza kwamba, mwaka huuu pia watu watashiriki kwa hamasa kubwa katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds kwa sababu tukio hili lina umuhimu maalumu kwao na litapelekea kudhoofika utawala haramu wa Israel ambao unaelekea kusambaratika.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran ameashiria wasi wa mwisho wa Imam Ali bin Abi Twalib (AS) na kusema: Maandamano ya Siku ya Quds yanakumbusha kumsaidia madhulumu na kupinga kudhulumu na kutekeleza wasio huo ndio ile nara ya "Mauti kwa Israel.

Ayatulah Khatami ameashiria katika sehemu nyingine ya hotuba zake juu ya kugonga mwamba na kushindwa mipangu michafu ya maadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kuhusiana na makubaliano ya hivi karibuni ya Iran na Saudi Arabia ya kuhuisha uhusiano wa kidiplomasia baina yao, khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema, baada ya makubaliano hayo, hivi sasa kuna mataifa ambayo yamepanga safu ya makubaliano.

Ameashiria pia kushindwa na kufeli njama za Marekani za kuanzisha kambi ya mataifa ya Kiarabu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

4132043

captcha