IQNA

Utamaduni wa Kiislamu

Jumba la Makumbusho la Berlin laonesha "Sanaa ya Kiislamu" kidijitali + Video

21:29 - February 25, 2023
Habari ID: 3476624
TEHRAN (IQNA)- Tovuti mpya ya Jumba la Makumbusho la Berlin la Sanaa ya Kiislamu ni jukwaa la kwanza la kidijitali katika ulimwengu unaozungumza Kijerumani kuwasilisha tamaduni za Kiislamu kwa njia ya kibunifu na ya kuburudisha.

Siku hizi, wale wanaotaka kupata uzoefu wa sanaa na utamaduni wa ulimwengu wa Kiislamu si lazima tena watembelee Jumba la Makumbusho la Sanaa ya Kiislamu la Berlin, ambalo lina kazi mbalimbali za sanaa za Kiislamu zilizochukua karne na mabara.

Katika sehemu ya juu ya Pergamon, jumba hilo la makumbusho limebuni "Sanaa ya Kiislamu" - jukwaa la kwanza la mtandaoni katika ulimwengu unaozungumza Kijerumani kuwasilisha nyenzo kuhusu tamaduni za Kiislamu kwa njia ya Kijerumani, Kiingereza na Kiarabu kwa njia ya kuburudisha.

"Sanaa ya Kiislamu" inakupelekea katika zama za kale. Kutoka eneo la uchimbaji wa kale huko Samarra nchini Iraq hadi mkusanyiko wa zulia kwenye Makumbusho ya Bode ya Berlin hadi kwenye kapu la Alhambra kutoka kilele cha utamaduni wa Kiislamu huko Andalucia. Lengo la jukwaa hilo, anaeleza mkurugenzi wa jumba la makumbusho Profesa Stefan Weber, ni kuwapa watu wengi iwezekanavyo, bila kujali ujuzi wao wa kielimu, fursa ya kugundua tamaduni za Kiislamu kwa njia ambayo inahimiza kuthamini utofauti wao. Na hii inapaswa kutokea kwenye kwenye jumba la makumbusho lenyewe, na nje ya jumba hilo katika vituo vya elimu na pia mtandaoni katika vyombo vya habari vya dijitali.

Anasema jumba hilo la makumbusho linazingatia visa mbali mbali na ujumbe wa visa hivyo katika zama zetu sambamba na utajiri wa kiutamaduni wa Uislamu.

Aidha Weber anabaini kuwa, maendeleo mengi ya kitamaduni katika jamii za Kiislamu za enzi ya kabla ya kisasa - miingiliano muhimu zaidi ya historia ya kitamaduni ya kimataifa kati ya Mashariki ya Kati, Afrika, Ulaya, Asia ya Kati, India, Mashariki ya Mbali na Uchina  huathiri maisha yetu hadi leo hii. Malengo mengine ya jukwaa hilo ni kukabiliana na viwango vinavyoongezeka vya chuki dhidi ya wahamiaji na Waislamu, anasema.

4124167

captcha