IQNA

Jumuiya za Kiislamu Ulaya zalaani kuvunjia heshima Qur'ani nchini Sweden

12:31 - April 18, 2022
Habari ID: 3475139
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Vituo vya Kiislamu Ulaya imelaani kitendo cha kuvunjiwa heshim Qur'ani Tukufu nchini Sweden hivi karibuni.

Rasmus Paludan, raia wa Denmark ambaye ni kinara wa chama chenye misimamo mikali cha Stram Kurs nchini Sweden aliteketeza moto nakala ya Qur'ani Tukufu katika mji wenye Waislamu wengi siku ya Alhamisi.

Paludan, akiwa ameandamana na maafisa kadhaa wa polisi, alienda katika uwanja uliowazi katika mji wa Linkoping kusini mwa Sweden ambapo alitekeleza kitendo hicho kiovu. Pludan pia alikuwa amepanga kuteketeza nakala za Qur'ani katika miji kadhaa ya Sweden wakati wa siku kuu ya pasaka.

Kufuatia kitendo hicho taarifa ya jumuiya hiyo imetoa wito wa kuheshimiwa matukufu ya Kiislamu kueshimiwa sambamba na kubainisha wasiwasi wake kuwa vitendo kama hivyo vinaumiza hisia za Waislamu.

Jumuiya ya Vituo vya Kiislamu Ulaya imetahadahrisha kuwa vitendo vya kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu hueneza hofu na kuibua mifarakani katika jamii.

Aidha jumuia hiyo imesema vitendo kama hivyo visivyo vya kistaarabu ni kinyume cha misingi ya haki za binadamu, heshima kwa dini za Mwenyezi Mungu na kuishi pamoja kwa maelewano raia wote.

Jumuiya ya Vituo vya Kiislamu Ulaya imetoa wito kwa vijana Waislamu wasitumbukie katika mtego wa mapigano kwani hilo ndilo makundi ya wazungu wenye misimamo mikali yanataka.

4050190

captcha