IQNA

Shule ya Waislamu yahujumiwa nchini Sweden

21:18 - March 15, 2021
Habari ID: 3473737
TEHRAN (IQNA)- Shule moja ya Waislamu kati mwa Sweden imeshambuliwa na watu wasiojulikana.

Hussein Aldaodi, mkuu wa shule ya Alsalamskolan iliyo katika mkoa wa Orebro amesema kamera za siri zimeonyesha watu wawili wakiwasha moto kwa lengo la kuitetekteza shule hiyo.

“Watu wawili waliokuwa wamefunika nyuso zao kwa barakoa walivunja madirisha ya shule na kuwasha moto,” amesema Aldaodi.

Amesema moto haukunea na hakuna aliyejiruhiwa katika tukio hilo kwani hapakuwa na mtu yeyeote shuleni wakati huo. Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu tuukio.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na hujuma  dhidi ya Waislamu nchini Sweden na maeneo mengine ya Ulaya.

3959705

Kishikizo: sweden waislamu
captcha