IQNA

Ujerumani yakosolewa kwa kuipiga marufuku Hizbullah

20:51 - May 02, 2020
Habari ID: 3472727
TEHRAN (IQNA) – Ujerumani imeendelea kukosolewa kutokana na hatua yake ya kuipiga marufuku Harakati ya Hizbullah ya Lebanon.

Weledi wa mambo ya kisiasa wamesema hatua hiyo ya wakuu wa Berlin kutangaza Harakati ya Hizbullah kuwa ni kundi la kigaidi kutapelekea Ujerumani ipoteze itibari katika eneo la Asia Magharibi.

Wakati huo huo, Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina imelaani hatua ya Ujerumani ya kuiweka Hizbullah ya Lebanon kwenye orodha ya makundi ya kigaidi na kueleza kwamba hatua hiyo inadhihirisha upendeleo na uungaji mkono wa Berlin kwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Taarifa iliyotolewa na harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina imebainisha kuwa, uamuzi huo wa Ujerumani umechukuliwa kukidhi matakwa na mashinikizo ya Marekani na utawala wa Kizayuni na ni tishio la kudumu kwa amani na uthabiti wa eneo.

Harakati hiyo ya muqawama ya Palestina imesisitiza katika taarifa yake hiyo kuwa, Hizbullah ya Lebanon ni moja ya nguzo kuu za muqawama katika kukabiliana njama za kila mara zinazofanywa na utawala wa Kizayuni kwa lengo la kuishambulia kijeshi ardhi ya Lebanon na ikabainisha kuwa, uamuzi wa Ujerumani wa kuupendelea na kuuunga mkono utawala wa Kizayuni unapingwa kikamilifu na wananchi wa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu na watetezi wote wa uhuru na kujitawala duniani kote.

Wakati huohuo Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS nayo pia imelaani hatua ya Ujerumani ya kuiweka Hizbullah ya Lebanon kwenye orodha ya makundi ya kigaidi.

Taarifa iliyotolewa jana pia na msemaji wa Hamas Hazim Qassem imelaani hatua ya kiuadui ya Ujerumani ya kuitambua Hizbullah ya Lebanon kuwa ni kundi la kigaidi na ikabainisha kwamba, uamuzi huo wa Ujerumani unaonyesha upendeleo na uungaji mkono wa wazi kabisa kwa mtazamo wa wavamizi ambao wangali wanaendeleza uchokozi na mauaji dhidi ya mataifa ya Kiarabu.

Juzi Alkhamisi, katika hatua ya kuupendezesha na kuuridhisha utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani, serikali ya Ujerumani iliitangaza Hizbullah kuwa ni kundi la kigaidi na kupiga marufuku shughuli za harakati hiyo ya muqawama wa Kiislamu katika ardhi ya nchi hiyo.

3895667

captcha