Mashindano hayo ambayo pia yanajulikana kama Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Sheikh Fatima Bint Mubarak yanatazamiwa kuanza Novemba 1.
Ibrahim Mohamed Bu Melha, mshauri wa Mtawala wa Dubai katika masuala ya utamaduni na ambaye pia ni mwenyekiti wa Zawadi ya Kimataifa ya Qur'ani ya Dubai (DIHQA) ambayo huandaa mashindano hayo ,amesema mashindano ya mwaka huu yanatazamiwa kuanza Novemba 1.
Amesema duru tatu zilizopita za mashindano zilifanyika kwa mafanikio kwa ambapo zilikuwa na wawakilishi wa nchi 72, 76 na 75 kwa taratibu.
Wanaotaka kushiriki katika mashindano hayo wanapaswa kuwa na umri wa chini ya miaka 25 na wawe na uwezo wa kuzingatia misingi ya Tajwidi.
Washindi watapokea zawadi za fedha taslimu 250000, 200000 na 150000, kwa taratibu Dirhamu za Imarati.
Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran atakuwa ni Binti Zainab Feyzi, mwenye umri wa miaka 8 kutoka Tehran.