Aida Hadzialic ambaye ni Msweden mwenye asili ya Bosnia amehitimu kwa shahada ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Lundi na aliwahi kuwa naibu meya wa mji wa Halmstad nchini Sweden akiwa na umri wa miaka 23. Alizaliwamwaka 1987 huko Foča, Bosnia, na kuteuliwa huko kunamfanya mwanasiasa mwenye umri wa chini zaidi nchini Sweden kuwahi kuteuliwa kuwa waziri.
Hadzialic alikuwa na umri wa miaka mitano wakati familia yake ilipokimbia kutoka vita vya Bosnia-Herzegovina.
Ikumbukwe kuwa Bosnia ilitumbukia katika vita vya ndani mwaka 1992 ambapo watu laki mbili waliuawa na mamilioni ya wengine kuachwa bila makao wakati vikosi vya Waserb vilipoanzisha mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu wa Bosnia.
Asilimia 15 ya raia wote wa Sweden walizaliwa katika nchi za kigeni. Inakadiriwa kuwa Waislamu ni karibu nusu milioni kati ya watu wote milioni tisa nchini humo.../mh