Taasisi ya Minhaj al-Qur'an ya Pakistan imepanga kuendesha mafunzo ya Qur'ani Tukufu katika maeneo 500 ya nchi hiyo maalumu kwa ajili ya mieizi mitukufu ya Shaaban na Ramadhani.
2012 Jun 20 , 17:26
Mwakilishi wa Ujerumani katika Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu amesema kiwango cha mashindano ya mwaka huu kimeimarika ikilinganishwa na miaka iliyopita.
2012 Jun 20 , 17:17
Mwakilishi wa Ufaransa katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tehran:
Qarii na mwakilishi wa Ufaransa katika Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu mjini Tehran amesema washiriki wengi katika mashindano hayo ya kimataifa ni vijana na kubainishiwa vijana hao misingi ya mwamko wa Kiislamu ni sawa na kufikisha ujumbe kwa jamii zao.
2012 Jun 19 , 18:02
Mashindano ya kiraa ya Qur'ani Tukufu maalumu kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani yamepangwa kutangazwa moja kwa moja kupitia redio ya Sayoun nchini Yemen.
2012 Jun 19 , 17:33
Warsha ya mafunzo ya Qur'ani Tukufu na sayansi ya Qur'ani makhsusi kwa ajili ya walimu imefanyika katika kituo cha mji wa Fathiyye nchini Uturuki.
2012 Jun 19 , 17:28
Duru ya 12 ya mashindano ya kitaifa ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu yalianza jana Jumapili huko Yemen kwa kuwashirikisha washindani 160 wa kiume na kike.
2012 Jun 19 , 17:18
Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yameanza Jumapili hapa mjini Tehran yakishirikisha mahafidh na maqari kutoka karibu nchi 70 za mabara matano ya dunia.
2012 Jun 18 , 10:08
Kongamano la tatu la kuwaenzi wanawake wanaharakati katika masuala ya Qur’ani Tukufu litafanyika Juni 30 pembizoni mwa Mashindano ya 29 ya Qur’ani Tukufu ya Iran mjini Tehran.
2012 Jun 17 , 16:37
Qur'ani ya kwanza iliyoandikwa kwenye jiwe duniani ambayo imeandikwa na msanii wa Iran ambaye ni mlemavu wa vita vya kulazimishwa vya Iraq dhidi ya Iran, itaonyeshwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
2012 Jun 16 , 19:22
Katika safari yake ya hivi karibuni huko Kabul mji mkuu wa Afghanistan, Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC ametembelea na kushuhudia kwa karibu Qur'ani kubwa zaidi duniani inayoonyeshwa katika Kituo cha Utamaduni cha Hakim Nasr Khosro Balkhi mjini humo.
2012 Jun 16 , 19:13
Duru ya tisa ya mashindano ya kimataifa ya tafsiri na kiraa ya Qur'ani Tukufu imepangwa kufanyika katika mtaa wa Dar al-Imam katika mji mkuu wa Algeria, Algiers tokea tarehe 8 hadi 14 Agosti.
2012 Jun 16 , 19:08
Mwanaharakati wa Qur'ani Senegal:
Waislamu wa Senegal hutumia mbinu mbalimbali kwa ajili ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu lakini mbinu ya kugawa Qur'ani katika sehemu tatu zenye juzuu 10 kila moja iliyotayarishwa na Abdulmuhsin al Qasim ambaye ni khatibu wa Masjidunnabi (saw) mjini Madina ndiyo yenye wafuasi wengi kutokana na kubakisha aya za kitabu hicho daima katika bongo za mahafidhi wa Qur'ani.
2012 Jun 14 , 13:39
Mafunzo maalumu ya tabia za Qur'ani Tukufu yatatolewa hivi karibuni kwa madereva wote wa Shirika la Taksi la Dubai (DTC) na Idara ya Usafiri wa Mikoani (RTA).
2012 Jun 12 , 17:22