Washiriki katika mashindano ya hifdhi ya Qur’ani Tukufu makhsusi kwa ajili ya wasichana huko Dubai wameanza kujiandikisha leo Jumanne.
2012 Jul 10 , 17:36
Idadi kubwa ya Waislamu Finland wanajiunga na madrasa za Qur’ani kwa lengo la kuimarisha imani yao ya kidini, amesema professor Jaakko Hämeen-Anttila mtafiti wa masuala ya Uislamu katika Chuo Kikuu cha Helsinki.
2012 Jul 10 , 17:06
Shirika la Wakfu katika mkoa wa Kermanshah nchini Iran limeandaa vikao kadhaa vya Qur’ani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ambavyo vitawashirikisha maqarii wa Qur’ani kutoka Misri.
2012 Jul 10 , 16:47
Sherehe za kushukuru na kuwaenzi mahafidh wa Qur'ani Tukufu zimefanyika katika msikiti wa Ijumaa wa mji wa Tortum ulioko katika mkoa wa Erzurum nchini Uturuki.
2012 Jul 09 , 13:00
Ratiba kadhaa zenye maudhui ya miujiza ya kisayansi ya Qur'ani Tukufu zimetekelezwa katika nchi za Kiafrika kwa usimamizi wa Kamati ya Kimataifa ya Muujiza wa Qur'ani na Suna za Mtume (saw) iliyo chini ya Jumuiya ya Kimataifa ya Uislamu.
2012 Jul 08 , 17:29
Idara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Imarati imeanza kukusanya nakala za Qur'ani Tukufu zilizochapishwa bila ya ruhusa ya vyombo husika.
2012 Jul 08 , 12:11
Kalamu ya elektroniki na simu ya mkononi makshsusi kwa ajili ya kusoma Qur'ani Tukufu vimeanza kuuzwa nchini India kwa mnasaba wa kukaribia mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa ajili ya kutayarisha uwanja mzuri kwa wasomaji wa kitabu hicho.
2012 Jul 07 , 21:27
Mafunzo ya kiraa na hifdhi ya Qur'ani Tukufu kwa wanachuo wa Kishia nchini Pakistan yamepangwa kuanza kutolewa siku ya Jumapili Julai 22 hadi Ujumaa tarehe 10 Agosti katika mji wa Jalalpur ilioko katika jimbo la Punjab.
2012 Jul 07 , 17:14
Sherehe za ufunguzi wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu zilifanyika hapo jana usiku katika Kituo cha Kibiashara ya Kimataifa cha Malaysia mjini Kuala Lumpur.
2012 Jul 07 , 16:59
Mahafidh bora wa Qur'ani Tukufu walishukuriwa na kuenziwa siku ya Jumatatu huko katika mji wa Elbista nchini Uturuki.
2012 Jul 05 , 06:21
Duru ya kwanza ya mashindano ya Qur'ani Tukufu nchini Ufaransa yatatangazwa moja kwa moja kupitia redio Pastel FM.
2012 Jul 04 , 12:59
Jumuiya ya Kimataifa ya Wanafunzi Waliohitimu Masomo yao Al-Azhar nchini Misri imetoa mwaliko kwa wanafunzi wa kigeni waliohitimu masomo yao katika chuo hicho cha kidini kuandikisha majina yao hadi kufikia tarehe 15 Julai kwa ajili ya kushiriki kwenye mashindano ya Qur'ani Tukufu yanayotazamiwa kufanyika hivi karibuni nchini humo.
2012 Jul 04 , 12:59
Mahafali ya kimataifa ya kufarijika na Qur'ani Tukufu imefanyika hivi karibuni katika Haram ya Imam Hussein (as).
2012 Jul 03 , 17:32