IQNA

Mtume Muhammad SAW

Kampeni ya ‘Mtume kwa Wote’ yazinduliwa na Waislamu wa Mumbai

22:39 - September 28, 2022
Habari ID: 3475848
TEHRAN (IQNA) - Mashirika na vikundi vya Kiislamu huko Mumbai nchini India vimeanza kampeni ya kukuza mafundisho ya Mtume Muhammad (SAW) katika mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.

Huku Waislamu wakiukaribisha mwezi wa Rabi-al-Awwal, mwezi ambao Mtume Muhammad (SAW) alizaliwa, baadhi ya mashirika na vikundi vya Kiislamu mjini Mumbai vimeanzisha kampeni mpya ya kueneza mafundisho na mahubiri ya Mtume Muhammad (SAW) kwa lengo la kuondoaa dhana potofu kuhusu Uislamu.

"Kampeni ya Mtume kwa Wote", inajumuishaa misikiti mbalimbali, madrasa, shule au vyuo vinavyoendeshwa na Waislamu, NGOs, mashirika ya kijamii na kitamaduni, na vyombo vingine vya Waislamu.

“Hili si zoezi la kiinjilisti. Tuna nia tu ya kufikisha ujumbe wa Mtume Muhammad SAW wa upendo, amani na udugu kwa ndugu zetu wote wasio Waislamu ili waweze kuwa na  ufahamu bora wa Uislamu na wafuasi wake," kiongozi wa kampeni hiyo  Yusuf Abrahani, ambaye pia ni Rais wa Islam Gymkhana, amesema.

Ubinadamu kwa Jumla

Kando na kubainisha kuwa ujumbe wa Mtume Muhammad (SAW) ni kwa wanadamu wote, kampeni hiyo itazingatia kutunza mazingira, kuhifadhi maji, huruma kwa masikini, wasiojiweza, mayatima, vibarua na wanawake.

"Kuna takriban misikiti 500 huko Mumbai, karibu shule 400 na vyuo 20 ... katika kampeni," alibaini Aamir Edresy, rais wa Chama cha Wanataaluma wa Kiislamu (AMP).

"Tunatuma maombi kupitia wanafunzi kwa familia zao kushiriki katika kampeni, kualika angalau wenyeji watano au majirani nyumbani kwao kwa chakula mnamo Oktoba 9, na kujaribu kufikisha ujumbe wa Mtume(SAW). Aidha kampeni pia itafanyika kwenye mitandao ya kijamii. ,” Edresy ameongeza

Qur’ani imejaa matukio mengi kuhusu sifa za kipekee za   wa Mtume Muhammad (SAW), mojawapo ikiwa ni aya ifuatayo:

Qur’an inasema: “Na hatukukutuma wewe (Ewe Muhammad) ila uwe ni rehema kwa  walimwengu wote.” Sura Al Anbiya-107.

Mapema mwaka huu, Baraza la Wazee wa Kiislamu lilianzisha kampeni mpya inayoangazia ujumbe wa wa Mtume Muhammad (SAW) uliojaa  amani na upendo kwa binadamu.

Kampeni ya #Prophet_of_Humanity iliwashirikisha wanazuoni mbalimbali wakuu wa Kiislamu kuhusu ujumbe wa Mtume Muhammad (SAW) kwa ulimwengu.

3480644

captcha