IQNA

Jinai za Israel

Wanajeshi wa Israel wamuua Mpalestina baada ya Sala ya Alfajiri

20:22 - August 19, 2022
Habari ID: 3475648
TEHRAN (IQNA) – Vikosi vya kijeshi vya utawala haramu wa Israel vimemuua Mpalestina mmoja katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan alipokuwa akitoka msikitini kuelekea nyumbani kwake baada ya Sala ya Alfajiri

Salah Sawafta, 58, alipigwa risasi kichwani katika mji wa Tubas siku ya Ijumaa asubuhi, Shirika la Hilali Nyekundu la Palestina lilisema.

Alipata matibabu ya dharura kabla ya kupelekwa hospitali ambapo hali yake ilielezwa kuwa mbaya.

Saa chache baadaye, Wizara ya Afya ya Palestina ilitangaza kuwa amekufa.

Meya wa Tubas, Hossam Daraghmeh, alisema Sawafta alikuwa akitoka kwenye Sala ya Alfajiri alipopigwa risasi.

“Alitoka msikitini na kuelekea nyumbani kwake akiwa amevaa vazi la kuswalia, kulikuwa na askari mwenye nia mbaya aliyekuwa amejipanga katika jengo lililo karibu na manispaa ambaye alimpiga risasi kichwani,” alisema.

Daraghmeh alisema Sawafta hakuwa na silaha kabisa.

“Mtu huyu hakuwa na jiwe wala kitu chochote mkononi,” alisema.

Wanajeshi wa Israel pia walimpiga risasi kijana mmoja kwa risasi moja kwenye paja la Tubas.

Wakati huo huo, Wapalestina walizuiliwa wakati wa maandamano katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa muda wote wa Alhamisi jioni na Ijumaa asubuhi.

Wapalestina watano, akiwemo mwanafunzi wa chuo kikuu, walikamatwa huko Tubas, kulingana na Jumuiya ya Wafungwa wa Palestina.

Huko Jenin, askari waliokuwa na silaha nzito katika kizuizi cha Za'tara, kusini mwa Nablus, walisimama na kuwaweka kizuizini vijana wawili kutoka mji wa Qabatiya, kusini mwa Jenin.

Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wanakabiliwa na vitisho vya kila siku, ghasia, na vikwazo kwa shughuli za kila siku kutoka kwa walowezi wa Kizayuni na askari wa vikosi vya utawala dhalimu wa Israel, ambao katika wiki za hivi karibuni wameongeza mashambulizi mabaya dhidi ya Wapalestina.

captcha