IQNA

Pazia al-Kaaba (kiswa) liko tayari+ PICHA

TEHRAN (IQNA)- Mchakato wa kushona na kutayarisha pazia jipya la Kaaba ambalo ni maarufu Kiswa umekamilika na pazia la zamani litaondolewa na jipwa kuwekwa tarehe Mosi Muharram 1444 Hijria Qamaria ambayo itasadifiana na July 29, 2022.
Kiswa ni pazia nyeusi ambayo hushonwa kwa hariri yenye uzito wa kilo 670 ambapo aya za Qur'ani hushonwa kwa uzi wa dhahabu katika pazio hilo.  Aya hizo hushindwa kwa dhahabu yenye uzito wa kilo 120 na uzi wa fedha wenye uzito wa kilo 100.