IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Marekani itazama kama ilivyozama meli kubwa ya Titanic

17:51 - February 18, 2020
Habari ID: 3472484
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei amesema Marekani itazama kama ilivyozama ile meli kubwa maarufu ya Titanic.

Marekani itazama kama ilivyozama meli kubwa ya TitanicAyatullah ameyasema hayo leo mjini Tehran mbele ya hadhara ya maelfu ya wananchi wa Azarbaijan Mashariki huko kakazini mwa Iran waliokwenda kuonana naye.

Akieleza jinsi Marekani inavyozidi kudhoofika siku baada ya nyingine, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, nchi hiyo imejiremba na kuitia vipodozi sura yake ya kidhahiri na kuongea kuwa: Marekani ambayo hii leo inadaiwa dola trilioni 22 inahesabiwa kuwa nchi yenye deni kubwa zaidi duniani, na tofauti za kimatabaka nchini humo zinatisha na ndizo kubwa zaidi kuliko kipindi kingine chochote.

Ayatullah ameashiria takwimu za kutisha za ubaguzi, tofauti iliyopo baina ya matabaka, umaskini na uhalifu nchini Marekani vinavyoangamiza uhai nchini humo mithili ya ukoma na kusema: Kama ambavyo haiba na ukubwa wa meli maarufu ya Titanic havikuzuia kughariki kwa meli hiyo, vivyo hivyo, juhudi za kurembesha sura ya dhahiri ya Marekani na haiba yake havitazuia kughariki nchi hiyo."

 Titanic ilikuwa meli kutoka Uingereza iliyojengwa kati ya 1909 na 1912 huko Belfast. Wakati ule ilikuwa meli kubwa duniani pamoja na mwenzake "Olympic". Ilipangwa kuzunguka kwenye Atlantiki kati ya Uingereza na Marekani.

Kwenye safari yake ya kwanza iligongana na siwa barafu tar. 14 Aprili 1912 mnamo saa sita kasorobo usiku ikazama baada ya masaa 2 na dakika 40 katika usiku wa tar. 15. Aprili.

Uchaguzi wa Bunge Iran

Kwenye sehemu nyingine ya hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei amesema kuwa kushiriki kwenye uchaguzi ni wajibu wa kidini, kitaifa na kimapinduzi na haki ya kiraia ya wananchi wote.

Ameashiria nguzo mbili muhimu za "mahudhurio makubwa ya wananchi" na 'kuchagua mtu anayefaa" na kusema: Kushiriki kwenye uchaguzi ni jihadi ya umma, neema na mtihani wa Mwenyezi Mungu ambao pale unapoandamana na mahudhurio ya idadi kubwa ya wananchi hulinda heshima ya Mfumo wa Kiislamu, kuimarisha nchi na kuipa kinga mbele ya njama (za maadui) na kutayarisha mazingira ya kujenga Iran yenye nguvu kubwa zaidi.

 Amesisitiza kuwa, macho ya marafiki na maadui yameelekezwa kwenye uchaguzi wa tarehe 21 Februari hapa nchini na kuongeza kuwa: Njia pekee ya kuwavunja moyo maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ni kuwa na Iran imara na yenye nguvu, na moja ya vielelezo vya Iran imara ni Bunge imara linaloweza kupasisha sheria zinazohitajika na kuilinda nchi kwa kuiongoza serikali katika njia inayofaa.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria baadhi ya ripoti zinazosema kuwa, mojawapo ya nchi kaidi za Ghuba ya Uajemi zimetoa kiwango kikubwa cha dola, fedha za mafuta, kwa chombo kimoja cha habari cha Uingereza kinachotangaza kwa lugha ya Kifarsi kwa ajili ya kuwashwishi Wairani ili wasiwachague wagombea wenye mielekeo na itikadi za kimapinduzi na kuongeza kuwa: Ripoti hiyo inaonesha ni kwa kiwango gani ubora na jinsi ya kuchagua vilivyo na umuhimu mkubwa.

Bwabwaja za Marekani

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Ayatullah Khamenei amezungumzia bwabwaja za hivi karibuni za maafisa wa serikali ya Marekani kuhusu Iran na uchaguzi na kusema: Marekani ilitaka kulidhibiti eneo la magharibi mwa Asia kupitia mauaji yake ya kigaidi dhidi ya Kamanda Qassem Soleimani ambayo yalikuwa na taathira kubwa katika eneo hilo, lakini mambo yalikwenda kinyume na lengo hilo; na maandamano makubwa yaliyofanyika dhidi ya Marekani mjini Baghdad, masuala ya Syria na Aleppo na kadhia nyingine za kanda hii vimekwenda kinyume kabisa na matakwa ya Wamarekani.

Ayatullah Ali Khamenei amesema adui hakupata pigo katika tukio la mauaji ya kigaidi ya Shahidi Soleimani pekee bali daima amekuwa akipata vipigo na kushindwa mbele ya taifa la Iran katika vita vya kipindi cha miaka 40 iliyopita. Ameongeza kuwa, katika kipindi cha miaka 40 iliyopita Wamarekani wametumia silaha zote za kisiasa, kijeshi, kiusalama, kiuchumi, kiutamaduni, vyombo vya habari na kila wenzo uliopatikana kwa ajili ya kuangusha utawala wa Kiislamu hapa nchini lakini Mfumo wa Kiislamu haujaondolewa madarakani, na kinyume chake, umeimarika zaidi mara elfu moja na Marekani imedhoofika kuliko hapo kabla.

3879593

captcha