IQNA

Malaysia kutayarisha chakula halali kwa ajili ya Olimpiki Tokyo 2020

21:15 - February 16, 2020
Habari ID: 3472477
TEHRAN (IQNA) –Malaysia imepewa jukumu la kutayarisha chakula halali, ambacho kimetayarishwa kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, kwa ajili ya michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020.

Moja kati ya viwandaa hivyo ni kile cha MyChef ambacho  kitayayarisha vyakula kama vile wali wa kukaanga, biryani ya kuku n.k na kukisafirisha hadi Japan kwa ajili ya kutumiwa na Waislamu watakaoshiriki katika michezo hiyo ya Olimpiki.

Mashirika ya Malayasia, ambayo ni nchi ya Kiislamu, yanatazamiwa kufaidika baada ya kupata kandarasi za kutayarisha chakula kwa ajili ya Waislamu watakaoshiriki katika michezo ya Olimpiki na Paralimpiki nchini Japan kuanzia Julai hadi Septemba mwaka huu.

"Ni fursa nzuri kwetu," amesema Ahmad Hussain Hassan, mkuu wa Shirika la MyChef ambalo linatayarisha vyakula hivyo katika mji wa Kual Lumpur.

Malaysia inalenga kutumia michezo ya Olimpiki mwaka huu kutangaza mashirika yake yanayotayarisha bidhaa halali. Uuzaji wa bidhaa halali Malaysia unatazamiwa kuiletea nchi hiyo pato la dola bilioni 12 mwaka huu.

Malaysia ndio nchi pekee ambayo imetia saini mkataba wa uuzaji bidhaa halali nchini Japan wakati wa michezo ya Olimpiki mwaka huu.

3470653

captcha