IQNA

Walowezi wa Kizayuni wauhujumu Msikiti wa Al Aqsa

10:31 - February 13, 2020
Habari ID: 3472467
TEHRAN (IQNA) – Makumi ya walowezi wa Kizayuni wameuhujumu Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa mujibu wa gazeti la Al Quds,  walowezi wa Kizayuni walipewa ulinzi na polisi ya utawala wa Israel wakati walipouhujumu na kuuvunjia heshima Msikiti wa Al Aqsa Jumatano.

Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu vinafanyika katika hali ambayo, viongozi wa nchi za Kiarabu zikiongozwa na Saudi Arabia, zinaendelea kujikurubisha kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa mujibu wa duru za Kipalestina, karibu kila siku walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakifanya uvamizi katika msikiti huo lengo likiwa ni kutekeleza njama za kutokomeza utambulisho wa Kiislamu na Kikristo wa Msikiti wa al-Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu, na badala yake kuweka nembo za Kizayuni.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.

Hata hivyo kusimama kidete wananchi wa Palestina hadi sasa kumekwamisha njama na mipango yote ya Wazayuni, zikiwemo njama zake za kubadilisha muundo wa kijamii na kijiografia wa Quds

Uvamizi huo unakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi ya Palestina. 

3470622

captcha