IQNA

Maandamano ya kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu kufanyika kote Iran katika miji na vijiji 5,200

18:21 - February 09, 2020
Habari ID: 3472453
TEHRAN (IQNA) - Maandamano makubwa ya 22 Bahman (11 Februari) katika kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yamepangwa kufanyika katika miji na vijiji 5,200 kote Iran.

Hayo yamedokezwa na Nasrullah Lotfi, Kaimu Mkuu wa Baraza la Uratibu la  Shirika la Tablighi ya Kiislamu nchini Iran. Akizungumza na waandishi habari mjini Tehran leo Jumapili, amesema mwaka huu maadhimisho ya 22 Bahman yamepewa jina la 'Mapinduzi ya Kiislamu Yako Hai Katika Nuru ya Kumfuata Faqihi Mtawala, Jihadi na Mapambano (Muqawama)".

Ameongeza kuwa, maandamano ya mwaka huu yataakisiwa na waandishi habari elfu sita Wairani na wa kigeni ambao watakuwa katika maeneo yote ya Iran.

Nasrullah Lotfi ameongeza kuwa, sifa ya kipekee ya maadhimisho ya mwaka huu ni kumuenzi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye aliuawa shahidi Januari 3 katika hujuma ya kigaidi ya Marekani nchini Iraq. Aidha amesema Rais Hassan Rouhani atahutubu katika maadhimisho hayo ya 22 Bahman mjini Tehran siku ya Jumanne.

Aidha amesema kesho Jumatatu usiku kutasikika nara ya Allahu Akbar kote Iran ambapo kutakuwa na maonyesho ya fataki mjini Tehran na baadhi ya miji ya Iran katika mkesha wa 22 Bahman.

Tarehe 11 Februari miaka 41 iliyopita Iran ikuwa katika siku ya kihistoria itakayokumbukwa siku zote. Siku hiyo wananchi waliokuwa wakipiga takbira na kutoa nara za kimapinduzi chini ya uongozi wa Ayatullah Ruhullah Khomeini walihitimisha kipindi cha giza totoro katika historia ya Iran kwa kuung'oa madarakani utawala wa kidikteta wa Shah Reza Pahlavi. Wananchi wanamapinduzi wa Iran, wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee na watu wa matabaka yote walisimama kidete wakipambana na mizinga na vifaru vya jeshi la Shah na kujisabilia kwa ajili ya Mapinduzi ya Kiislamu. Mapambano ya wananchi Waislamu wa Iran yalienea nchini kote huku wafuasi wa Imam Ruhullah Khomeini wakiwa katika juhudi za kumaliza kabisa mabaki ya utawala wa kidhalimu wa kifalme.

3877488

captcha