IQNA

Tarjuma ya Qur'ani kwa lugha ya Kiamhara yachapishwa

12:48 - May 24, 2019
Habari ID: 3471970
TEHRAN (IQNA)- Taasisi ya Kiislamu ya Diyanet (TDV) ya Uturuki imechapisha tarjuma ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kiamhara ya Waislamu wa Ethiopia.

Kwa mujibu wa taarifa nakala 15,000 za Tarjuma ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kiamhara zitasambazwa baad aya uchapishaji kukamilika kwa ushirikiano wa Idara ya Masuala ya Kidini ya Ofisi ya Rais wa Uturuki kama sehemu ya mradi wa 'Qur'ani iwe zawadi yangu' amesema Cemil Alici mshauri wa masuala ya kidini katika Ubalozi wa Uturuki mjini Addis Ababa.

Amesema nakala 6,000 zitasambazwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mradi wa tarjama hiyo umeungwa mkono na Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu Ethiopia nani muhimu kwa Waislamu wa Ethiopia.

Idadi ya watu wanaozungumza lugha ya Kiamhara, wanakadiriwa kufikia milioni 19.8, kiasi cha asilimia 26 ya wakazi wote wa Ethiopia. Hii ni kwa mujibu wa sensa ya taifa ya mwaka 2007. Huongea lugha ambayo imekuwa lugha ya wafanyakazi na taasisi za serikali na za jamii, pia ya siasa na uchumi nchini humo.

3468593

captcha