IQNA

Waziri Mkuu wa Malaysia: "Waislamu wanapaswa kuwa na ufahamu sahihi wa Qur'ani"

12:36 - March 18, 2019
Habari ID: 3471880
TEHRAN (IQNA) – Waziri Mkuu wa Malaysia Mahathir Mohammad amesema baadhi ya Waislamu hawana ufahamu sahihi wa Qur'ani na hivyo wanajihusisha na vitendo vilivyo kinyume cha mafundisho ya Uislamu.

Ameongeza kuwa Waislamu wanapaswa kuwa na ufahamu sahihi wa Qur'ani Tukufu na wasitosheke tu na uwezo wa kusoma au kuhifadhi kitabu hicho kitakatifu.

Akizungumza katika Mashindano ya Kitaifa ya Kusoma na Kuhifadhi Qur'ani mjini Banama, Machi 17, alifafanua zaidi amesema: "Hivi karibuni tumeshtushwa na mauaji ya kinyama ya Waislamu wenzetu 49 waliokuwa wakiswali katika misikiti miwili ya Christchurch (New Zealand). Hicho kilikuwa kitendo ambacho kimetekelezwa na gaidi aliyetaka kulipiza kisasi mauaji ya wasiokuwa Waislamu yaliyotekelezwa na Waislamu."

Mahathir amesema watu wasio na hatia kwa kawaida ndio ambao huwa wahanga wa hujuma hizo zilizojaa chuki.

"Watu 49 waliouawa misikitini hawakuwa na hatia na hawakujihusiha na vitendo vya utumiaji mabavu. Mauaji hayo yamewakasirisha Waislamu na baadhi watataka kulipiza kisasi."  Waziri Mkuu wa Malaysia amesema iwapo watu wataanza kulipiza kisasi, mauaji kama hayo hayatasita na hali itazidi kuwa mbaya.

Halikadhalika Waziri Mkuu wa Malaysia amesema kuna dhana potofu kuwa kuwa Mwislamu ataneda peponi kwa kuua katika hali ambayo dhana kama hivyo ni ufahamu usio sahihi wa Qur'ani.

3468159

captcha