IQNA

Serikali ya Morocco kukarabati misikiti 1,000

12:57 - November 29, 2018
Habari ID: 3471755
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Morocco imetangaza mpango wa kukarabati misikiti zaidi ya 1,000 nchini humo na imetaka ushirikiano wa sekta mbali mbali katika kufikia lengo hilo.

Waziiri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu Morocco Dkt. Ahmed Tawfiq ameyasema hayo katika sherehe iliyofanyika kwa lengo la kuenzi Siku ya Msikiti. Amesema kuwa misitiki 1,000 nchini Morocco inahitaji kukarabatiwa na imekadiriwa kuwa zoezi hilo litagharimu takribani dola milioni 105.

Dkt. Tawfiq ametoa wito kwa watu binafsi Morocco washiriki katika ukarabati wa misikiti hiyo ili iliyofungwa iweze kufunguliwa upya. Amesema badala ya kujenga misikiti mipya, kuna haja ya kukarabati misikiti ya kale.

Kwa mujibu wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Morocco,  misikiti 175 imejengwa nchini humo mwaka huu ambapo 160 imejengwa na watu binafsi na iliyosalia imejengwa na wizara ya wakfu.

3768010/

captcha