IQNA

Wanajeshi wa Saudia wahujumu Mashia katika maombolezo ya Muharram

12:04 - September 14, 2018
Habari ID: 3471670
TEHRAN (IQNA)- Wanajeshi wa utawala Saudi Arabia wamewashambulia Waislamu wa madhehebu ya Shia ambao walikuwa wakishiriki katika maombolezo ya Mwezi wa Muharram.

Kwa mujibu taarifa, tokea maombolezo ya Muharram yaanze Jumanne, wanajeshi wa Saudia wameharibu mahema zaidi ya 20 ya waombolezaji katika eneo la Qatif. Aidha wanajeshi wa Saudia wameondoa mango yaote yaliyokuwa yamewekwa mitaani kwa munasaba wa maombolezo ya Muharram.

Kwingineko, mtandao wa habari wa al-Ahd Lubnan, umefichua habari ya mwendelezo wa njama za utawala wa Saudia za kuvuruga maombolezo ya Muharram katika maeneo kadhaa nchini humo.

Mtandao huo umeripoti kuwa polisi nchini Saudia wamevamia Husseiniyah (ukumbi wa kidini)  ya eneo la al-Qadih na kutwaa vitu vilivyokuwa ndani yake, sambamba na kuharibu mimbari yake.. Mtandao wa habari wa al-Ahd Lubnan, umefichua habari ya mwendelezo wa njama za utawala wa Saudia kwa ajili ya ulipizaji kisasi dhidi ya wafuasi wa Ahlul-Baiti wa Mtume Muhammad SAW  katika miji ya Waislamu wa Shia.

Hayo yanajiri pamoja na kuwa,  Sheikh Wajdi Mubarak mmoja katia ya wanazuoni wa Kishia nchini Saudi Arabia alikuwa ametoa wito wa kuwepo ushirikiano kamili baina ya waumini na maafisa wa usalama nchini humo katika maadhimisho ya Siku ya Ashura. Mwanazuoni huyo wa Kishia nchini Saudia alisema maafisa wa usalama wana jukumu la kulinda usalama wa waumini wataoakoshiriki katika mijimuiko ya Muharram na Siku ya Ashura nchini humo.

Ikumbukwe kuwa, mwaka 61 Hijria Qamaria, moja kati ya vita mashuhuri katika historia ya Kiislamu na ya mwanadamu, vilitokea baina ya majeshi ya haki na batili katika ardhi ya Karbala huko Iraq.

Siku hii inajulikana kwa jina la Ashura. Katika siku hiyo mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib AS, alisimama kishujaa na wafuasi wake waaminifu 72, kukabiliana na jeshi kubwa la batili ili kuilinda dini ya Allah.

Katika siku kumi za kwanza za mwezi wa Muharram, Waislamu, hasa wafuasi wa Madhebu ya Shia na wale wawapendao Ahul Bayt wa Mtume SAW, hushiriki katika hafla mbali mbali za maombolezo ya Imam Hussein AS. Aidha hata wasio kuwa Waislamu katika maeneo mbali mbali pia hujumuika na Waislamu katika maombolezo ya Imam Hussein AS kwani aliuawa shahidi akitetea haki na kupinga udhalimu.

3466750

captcha