Magofu ya msikiti huo yametajwa kuwa ya zama za Ukhalifa wa Bani Abbas na yamepatikana karibu na falaj (njia za kumwagilia mashamba maji) na ulijumuisha kwa uchache majengo mtatu ya matofali.
Wanaakiolojia wa Idara ya Utamaduni na Utalii Imarati wanasema magofu ya msikiti huo yanaonyesha mihrabu ilivyokuwa na kwamba inakadiriwa kuwa waumini waliswali nje na ndani ya msikiti. Aidha wanaakiolojia wamepata mabaki ya vyungu ambavyo yamkini vilikuwa vikutumiwa kwa ajili ya maji ya udhuu au masuala mengine yanayohusiana na msikiti. Uchunguzi uliofanywa kwa kutumia mbinu ya radiocarbon umebaini kuwa msikiti huo ndio wa kale zaidi kuwahi kugunduliwa UAE hadi sasa.
3466725