IQNA

Kongamano la 'Zawadi ya Mtume wa Rahma' kufanyika Uganda

12:07 - June 24, 2018
Habari ID: 3471570
TEHRAN (IQNA)- Kongamano la 'Zawadi ya Mtume wa Rahma SAW' limepangwa kufanyika 30 Agosti mwaka huu kwa ushirikiano wa Baraza Kuu la Waislamu Uganda na Shirika la Utangazaji la Uganda, UBC.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maudhui kuu katika kongamano hilo itakuwa ni kubainisha Sira na Sunna ya Mtume Mtukufu wa Uislamu, Muhammad Al Mustafa SAW kama kigezo cha maisha ya leo. Kongamano hilo linatazamiwa kusisitiza kuhusu Mtume SAW kama kigezo katika suala la wafuasi wa dini mbali mbali kuishi pamoja kwa maelewano na umoja baina ya Waislamu katika Qur'ani na Sunna. Aidha mkutano huo utajadili namna ya kukabiliana na utumizi wa mabavu na misimamo mikali katika Sira ya Mtume wa Rahma SAW.

Wanaolenga kushiriki katika kongamano hilo wanatakiwa kutuma muhtasari wa makala zao kabla ya Julai Mosi na makala kamili kabla ya Agosti 8 ambapo makala bora zitatunikiwa zawadi Agosti 30.

Sherehe za kufunga kongamano hilo zinatazamiwa kuhudhuriwa na Mufti wa Uganda, waziri wa utamaduni wa nchi hiyo na maafisa wengine wa ngazi zajuu nchini humo katika Ukumbi wa Baraza Kuu la Waislamu Uganda.

3724518

captcha