IQNA

Mafuriko yatishia maisha ya wakimbizi 200,000 Waislamu Warohingya nchini Bangladesh

16:39 - June 17, 2018
Habari ID: 3471562
TEHRAN (IQNA)-Huku mvua za monsoon ziliendelea kunyesha katika kambi kubwa za wakimbizi Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Bangladesh, Umoja wa Mataifa umeonya kuwa maisha ya wakimbizi 200,000 yako hatarini.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumiwa watoto UNICEF linasema kambi za wakimbizi zinakabilia na mapromoko ya ardhi na maji yanazidi kupanda na hivyo kuna haja ya kuwahamisha watoto haraka.

Mvua za kwanza za msimi zilinyesha kwa wingi katika kambi za Cox's Bazar na mitaa ya mabanda katika eneo hilo. Mtoto moja alipoteza maisha kufuatia maporomoko ya ardhi, imesema taarifa ya UNICEF.

Kwa mujibu wa makadirio ya UNICEF zaidi ya makao 900 ya wakimbizi yaliharibiwa katika mvua hizo.

Mvua hizo zinatarajiwa kuendelea kwa wiki kadhaa na iwapo hatua hazitachukuliwa maafa hayo yataongozeka na yamkini idadi kubwa ya watu wakafariki au makao yao yataharibika. Baada ya mvua za monsoon kupungua mwezi Agosti eneo hilo litashuhudia kuanza msimu vya vimbunga na hivyo hali inatabiriwa kuzidi kuwa  mbaya zaidi.

Mbali na wakimbizi kupoteza maisha kutokana na kusmbwa na maji ya mafuruko pia kuna hatari ya kuenea magonjwa hatari kama vile kipindipindu.

Waislamu wa jamii ya Rohingya wamelazimika kukimbia kutoka ardhi zao za jadi nchini Myanmar na kutafuta hifadhi katika nji jirani ya Bangladesh kufuatia jinai kubwa wanazofanyiwa na wanajeshi na Mabudha wa nchi hiyo  wenye misimamo ya kufurutu katika mkoa wa Rakhine magharibi mwa nchi hiyo.

Wimbi jipya la jinai dhidi ya Waislamu Rarohingya  zilishika kasi tangu tarehe 25 mwezi Agosti mwaka jana. Hadii sasa  jina hizo zimepelekea kuuliwa Waislamu zaidi ya elfu sita na kujeruhiwa maelfu ya wengine huku wengine karibu laki nano wakilazimika kuwa wakimbizi katika nchi jirani ya Bangladesh.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa uhalifu unaofanywa na Mabudha kwa himaya ya serikali nchini Myanmar dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya ni mauaji ya kimbari.

Zeid Ra'ad Al Hussein anasisitiza kwamba, kuna udharura wa kufika katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na kufanya uchunguzi kuhusu ukatili unaofanywa na serikali ya Myanmar dhidi ya Waislamu.

3466081

captcha